WIZARA YA MALIASILI KUWAKAMATA WATUMIAJI VIBAYA WA MALIASILI

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kulia) akifurahia kinyago kilichochongwa na raia wa Afrika Kusini, Azwimpheleli (mwenye fulana nyeupe) huku Makamu wa Rais wa Chama cha Kimataifa cha Utamaduni wa Miti, Haward Rosen (mwenye tai) akimtazama.

Na Tulizo Kilaga

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema ataenda porini pamoja na jeshi lake kuwakamata wale wote wanaofanya matumizi mabaya yasio endelevu ya misitu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwenye kilele cha Siku ya Mbao Duniani, alisema serikali imeazimia kutoa elimu ya kutosha na kuwataadhalisha watu wenye nia mbaya, masilai binafsi ya kuchoma misitu kwa makusudi, kukata miti bila vibali na wale wanotolosha magogo.
Alisema tayari wameshaanza kuwakamata wananchi wanaohujumu misitu nchini na wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa lengo la kutaka wafungwe ili wawe fundisho kwa watu wasioitakia mema Tanzania.
Aliongeza kuwa watu wote wanaohusika na kuhujumu nchi kwa misitu ni wahujumu uchumi, na wahujumu uchumi hao watafuatwa kama ilivyokuwa kwenye zama za hayati Moringe Sokoine.

Aliongeza kuwa, serikali imeongeza nguvu kuhakikisha inaiokoa nchi dhidi ya janga la jangwa kwa kuamua kutumia maaskari wake wa misitu, wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vya nchi katika kupambana na ujangili wa wanyamapori na mazao ya misitu.
Nyalandu aliongeza kuwa, hali ilivyo sasa nchini kama watu hawatazamana machoni na kuambiana ukweli misitu ya Tanzania itatoweka yote. Hivyo alitoa wito kwa wanahabari na wananchi wote kushirikiana kuiokoa nchi dhidi ya janga la jangwa.
Akizungumzia maazimisho ya Siku ya Mbao Duniani yalioandaliwa na na Chama cha Kimataifa cha Utamaduni wa Miti alisema, Serikali imeazimia kuwaunganisha wasanii wote ili waweze kutengeneza kazi zenye ubora wa kimataifa utakaowawezsha kupenya kwenye soko la kimataifa.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Chama cha Kimataifa cha Utamaduni wa Miti, Haward Rosen aliwataka Watanzania kutumia mbinu za kitamaduni za kutumia miti na kutunza miti kama hazina.
Mwaka huu Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa siku Siku ya Kimataifa ya Miti kwa kuwa imeonyesha juhudi za kuwashirikisha wananchi wake katika kuhifadhi na kupanda miti.







Previous Post Next Post