Wilaya ya Kilwa yapokea walimu kukabiliana na changamoto la Elimu

picha (1)Walimu wapya wa shule za msingi na Sekondari ambao wameripoti na kupokelewa Wilayani Kilwa.picha (2)Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa akiwakaribisha walimu wapya
ulegaMkuu wa Wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega akitoa nasaha zake kwa walimu hao.
Abdulaziz LindiHALMASHAURI ya wilaya ya Kilwa imekabidhi meza nne za maabara
inayotembea kwa ajili ya mafunzo ya vitendo katika masomo ya
Baiolojia, Kemia , Kilimo na Fizikia kwa shule nne za sekondari ikiwa
ni sehemu ya hatua za kukabili changamoto za matokeo mabaya ya shule za sekondari za wilaya hiyo Hususan katika masomo ya sayansi.
Meza hizo zenye thamani ya shilingi Milioni 24 ikiwa ni awamu ya
kwanza ili ya kuziwezesha shule za zote za sekondari kuwa na Maabara zinazohamishika.
Tukio hilo lilioenda sambamba na kupokea walimu wapya wa shule za
msingi na Sekondari waliopangwa katika Halmashauri hiyo.
Akiongea katika katika hafla hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Abdallah
Ulega sambamba na kuwashukuru walimu hao kwa kufika wilayani humo Pia alitoa wito kwa Jamii kujenga Nyumba Bora hususan Vijijini ili kusaidia watumishi wanaopangwa huko kwa huduma za jamii zikiwemo Elimu na Afya kutokana na mazingira ya kusomea kutokuwa yenye mvuto ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa zana muhimu na maabara, na kwamba hatua ya kusambazwa kwa teknolojia hiyo rahisi licha ya kuwawezesha wanafunzi sasa kujifunza katika hali iliyobora zaidi kwa vitendo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Bw Addo Mapunda aliwasihi
walimu hao kufanya kazi kwa kuwa Wilaya hiyo inaupungufu mkubwa wa walimu hususan vijijini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw Ally  Mohamed Mtopa alitoa ahadi ya kununua kitanda na godoro kwa walimu watakaopangwa katika KATA yake lakini pia aliwageukia walimu hao kuhusiana na suala la migomo ya walimu ambapo aliwasihi kutojiingiza katika masuala hayo badala yake aliwaomba walimu hao kufikisha malalamiko yao kwa Madiwani ambao ndio wenye maamuzi ya Halmashauri hiyo Wilaya ya kilwa ilipangiwa jumla ya walimu 104 wa msingi na 78 wa Sekondari, Kati ya hao 7 hawajaripoti kwa shule za msingi huku sekondari walimu 23 hawajaripoti licha ya tarehe zilizowekwa na wizara kumalizika.
Previous Post Next Post