Na Lucy Mgina
KIUNGO wa kimataifa wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema ataangalia zaidi maslahi kabla ya kuamua kubaki au kuondoka Jangwani.
Niyonzima anatarajia kwenda nchini Tunisia kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ambayo hakutaka kuitaja huku mkataba wake Yanga ukiwa unaelekea ukingoni.
Akizungumza na Championi Jumatano, Niyonzima alisema kwa sasa anapigania kwanza timu yake itwae ubingwa wa ligi kisha baada ya hapo ataangalia hatima yake.
“Unajua kwenye mpira tunaangalia zaidi maslahi, hilo ndiyo jambo la msingi lakini pia nataka kuwa katika sehemu nzuri ambayo itanifanya nifanye kazi kwa ufasaha zaidi,” alisema Niyonzima.
Kiungo huyo ambaye alisajiliwa kutoka APR ya Rwanda amekuwa msaada mkubwa zaidi kwa Yanga msimu huu.
Tags
SPORTS NEWS