KOCHA wa Manchester United ameridhia beki wake Rio Ferdinand kujiunga na timu ya taifa.
Mwanzoni Ferguson alichukizwa na kitendo cha beki huyo mkongwe kuitwa timu ya taifa, lakini sasa kocha huyo amesema Rio atajiunga kwenye kikosi cha timu ya taifa Jumatatu.
Amesema Rio atapewa sapoti ya kutosha ya kimatibabu kwa muda wote atakao kuwa na timu ya taifa.
Hata hivyo Rio alikonekana kumpotezea Roy Hodgson na kuuchuna kupokea simu yake jambo lililomlazimiu kocha huyo wa timu ya taifa kuacha ujumbe wa sauti.
Rio 34, ameitwa tena timu ya taifa baada ya kuwa nje ya kikosi hizo kwa takriban miaka miwili.
Tags
SPORTS NEWS