MWENDELEZO WA TAMTHILIA YA SIRI YA MTUNGI IKIWA NI SEHEMU YA 11

Duma anaingia katika biashara yenye tija na Golden. Hata hivyo furaha yake ya maisha ya juu inakatizwa pale anapolazimika kushughulikia tatizo lililomkumba mdogo wake, Stephen. Matokeo ya kujamiiana ovyo na msichana muuza machungwa yanatisha. Kwa Duma, huu ni wito kwake kuchukua tahadhari zaidi za kumtunza mdogo wake.
Tula anaanza kumchoka Cheche anayemtumia wakati wowote anaopenda.
Siye Nusura peke yake anayetambua kuwa ni mja mzito. Taarifa ambayo ingeleta furaha inamwingiza matatani wakati Farida anatishia kufichua maisha ya "siri" ya Nusura yaliyopita ili aipate tena nafasi yake ya kwanza kwenye nyumba ya Mzee Kizito.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post