JENGO LA GHOROFA 16 JIJINI DAR LAANGUKA, WATU TAKRIBANI 60,WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA

Baadhi ya watu waliowahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha.Wahindi nao walikuwapo kutoa msaada.Waokoaji wakijitahidi kutumia mikono kuondoa kifusi hicho ili kuweza kuwaokoa watu waliofukiwa.
Trekta likiondoa kifusi eneo la ajali...Waokoaji wakiwa hoi.Juhudi zinaelekea kulalaMoja kati ya magari yaliyokuwa eneo hilo likiwa limeangukiwa na mabaki ya jengo hilo.
Taarifa zilizotufikia ni kwamba jengo lenye ghorofa 16 lililokuwa bado linaendelea kujengwa katika makutano ya barabara ya Indira Gandhi na Morogoro jirani na Burhani limeanguka. Inasemekana katika jengo hilo kulikuwa na watu takribani 60 ambao wanahofia kupoteza maisha. 488271_518827744827329_215924994_nRais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Previous Post Next Post