JE TAIFA STARS ITAENDELEZA REKODI YAKE YA KUTOPOTEZA MECHI NYUMBANI?

Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania 'Taifa stars' leo watakuwa na kibarua cha kuendeleza rikodi yao ya kutopoteza mchezo katika uwanja wa Taifa chini ya kocha Kim Poulsen watakapo wakaribisha Morocco 'simba wa atlas'.
Mchezo wa Tanzania na Moroco ni mchezo wa kusaka nafasi ya kushiriki kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil ambapo wako kundi moja na Ivory coast na Gambia.
Taifa stars imecheza michezo minne chini ya kocha Kim Poulsein katika uwanja wa Taifa mitatu ikiwa ni ya kirafiki na mmoja wa mashindano, ambapo wametoa sare mchezo mmoja na kushinda mitatu mfululizo.
Taifa stars inashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa kundi lake wakiwa na point 3 nyuma ya vinara Ivory coast wenye point 7 baada ya kuwafunga waburuza mkia Gambia hapo jana kwa jumla ya magoli 3-0, huku Moroco wakiwa wa 3 kwa kuwa na point 2.
Mara ya mwisho kwa Taifa stars kukutana na Moroco katika uwanja wa taifa ilikuwa mwaka juzi ambapo Moroco walitoka na ushindi wa goli 1-0 lililo fungwa na Shamack ambaye safari hii hayumo kikosini.
Tumaini la Tanzania lipo katika eneo la kiungo linaloundwa na Mwinyi Kazimoto, Franky Domayo, Salum Aboubakary wakisaidiana na Amiry Kiemba. Eneo hili limekuwa likicheza kwa uelewano mkubwa na kupelekea kuwa tishio kwa timu pinzani na kuwapa kazi nyepesi wa shambuliaji na walinzi wa stars.
Kikosi cha leo huenda kikawa hivi kulikana na mazoezi ya mwisho; JUMA KASEJA, ERASTO NYONI, SHOMARI KAPOMBE, AGGREY MORISE, KELVIN YONDAN, FRANKY DOMAYO, MRISHO NGASSA, SALUM ABOUBAKARY, MBWANA SAMMATA, MWINYI KAZIMOTO NA AMIR KIEMBA





Previous Post Next Post