ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE LINDI MJINI KATIKA PICHA.


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Lindi mjini, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akimsalimia mwananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara aliohutubia katika kijiji cha Nanyanje, Kata ya Chikonji wilayani humo leo, akiwa katika ziara ya siku saba kukagua na kuimarisha uhai wa Chama na Utekelezaji wa ilani.Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Chikonji, wakimsikiliza Mama Salma Kikwete alipozungumza nao katika kikao cha ndani, kwenye Ofisi ya CCM ya Kata hiyo.Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Lindi mjini, Mama Salma Kikwete mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nanyanje, wilaya ya Chikonji, wilaya ya Lindi mjini.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Mama Salma Kikwete akipokea kadi ya CUF kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa chama hicho, Salma Saidi (kushoto) baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Nanyanje, Kata ya Chikonji mkoani Lindi.Wanachama wapya wa CCM waliokabidhiwa kadi zao wakiwemo kutoka vyama vya CUF na Chadema, wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi zao na Mama Salma Kikwete.Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma ya zindiko ya wakazi wa Chikonji, iliyotumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo.Wasanii wa kundi la ngoma ya zindiko ya Chikonji wakionyesha umahiri wao katika mkutano huo.Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kijiji cha Nanyanje kata ya Chikonji mkoani Lindi.Wananchi wakiselebuka kwa nyimbo za CCM wakati wa mkutano huo.
Previous Post Next Post