YANGA Vs AZAM KESHO TAIFA

YAAZATimu ya Young Africans ambayo inaongoza msimamo wa Ligu Kuu ya Vodacom nchini VPL kwa kuwa na point 36 na mabao 33 ya kufunga na mabao 12 ya kufungwa kesho itashuka katika dimba la Uwanja wa Taifa kupambana na timu ya waoka mikate ya Azam FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.
Baada ya kuichapa timu ya African Lyon katika mchezo wake wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mabao 4-0, watoto wa Jangwani watashuka dimba la uwanja wa Taifa kesho kuhakikisha wanaondoka na point 3 muhimu na kuendeleza wimbi la ushindi mfululizo katika mzunguko wa pili wa Ligi ya Vodacom.
Kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kimeendelea na mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa mbegani pembeni kidogo ya mji wa Bagamoyo huku wachezaji wote wakifanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo huo utakaofanyika kesho lakini pia wakionekana kuwa wenye morali ya hali ya juu dhidi ya mchezo huo.
Kocha Mkuu Ernest mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi, amesema kikosi chake kipo tayari kabisa kuwavaa wauza lamba lamba Azam FC siku ya kesho, na katika kambi yao ya siku tatu mjini Bagamoyo imekua ni kambi nzuri na yenye maendeleo mazuri kwa wachezaji wake wote na benchi la ufundi.
Azam FC najiua ni timu nzuri, ina wachezaji wazuri lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kutuzuia sisi kuweza kuondoka na ushindi katika mchezo wa kesho, kwani pamoja na kuwa wao wana timu nzuri ila sisi tuna timu nzuri na bora zaidi kuliko timu yoyote katika ukanda huu wa Afrika Mashariki  'alisema Brandts'
Aidha kocha Brandts amesema wachezaji wake wote 26 wako katika hali nzuri, hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja katika kambi, na kesho atapata fursa ya kumtumia mchezaji yoyote kati yao katika kuhakikisha anaibuka na ushindi, kwani ameiandaa timu kuhakikisha inaondoka na poniti 3 katika mchezo huo.
Young Africans inahitaji kushinda mchezo wa kesho ili kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom ambapo mwishoni iweze kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu 2012/2013.


Vodacom Premier League 2013
Young Africans Vs Azam FC

Entrace:
VIP A Tshs 20,000/=
VIP B & C Tshs 15,000/=
Orange Tshs 8,000/=
Blue & Green Tshs 5,000/=





Previous Post Next Post