Watanzania wa Ujerumani kusheherekea miaka 49 ya Muungano.

Café Bühne und ShopWatanzania wa Ujerumani kusheherekea miaka 49 ya Muungano ,jumamosi 27-04-2013 Mjini Koln !

Umoja wa watanzania Ujerumani (U.T.U) Unapenda kuwajulisha kwamba Sherehe za miaka ya Muungano Wa Tanzania Bara na Visiwani zitafanyika mjini Koloni, ujerumani siku ya jumamosi Tarehe 27.04.2013 Kuanzia saa 8 za Mchana

katika ukumbi wa Circus Fabric uliopo katika anuani hii::-

Bergisch Gladbacher Strasse 1007a

51069 Köln

Vikundi mbali mbali vinatarajiwa kutumbuiza

Ufunguzi saa 8 mchana

Maigizo ya watoto

Sarakasi ya watoto

Sarakasi ya wakubwa

Ngoma za kiasili kutoka Tanzania

Break Dance

Live Bands

Maonyesho ya mavazi ya kisili ya kitanzania

Pia kutakuwa na chakula (a.k.a mnuso)

Kila mtanzania anaweza kushiriki kuuza bidhaa zake binafsi za sanaa kama Vinyago, picha,michoro, ususi NK. kuchukua nafasi katika ratiba ya maonyesho, wasanii wanaotaka kushiriki katika maonyesho wanatakiwa kujiandikisha moja kwa moja kwa Mwenyekiti wa UTU kupitia barua pepei ifuatayo-:

kamati.utu@googlemail.com

Cell: +491733 779720

Cell +491734297997

Umoja ni Nguvu! Utengano ni Udhaifu !

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post