Hata hivyo Jeshi la Polisi kupitia Vikosi vya Kutulia Ghasia-FFU-limelazimika kutumia Mabomu ya Machozi ili kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wamebeba Mabango na Mawe kwenye Mifuko katika Mitaa ya Malapa pamoja na Kariakoo.
mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umeshuhudia Maduka mbalimbali yakiwa yamefungwa katika Mitaa ya Kariakoo kutokana na maandamano hayo ya watu wanaodaiwa kuwa Waumini wa Dini ya Kiislam.
Waumini hao wanashinikiza Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka-DPP-kumwachia kwa dhamana Katibu wa Jumuiya ya Waislam Shekh PONDA ISA PONDA ambaye anakabiliwa na kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Jana Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar e s salaam kupitia kwa Kaimu Kamanda wake AHMED MSANGI lilipiga marufuku kufanyika kwa mandamano hayo kutokana na kutokuwa na kibali cha Polisi.
source: Mzee wa Matukio Daima
Tags
HABARI ZA KITAIFA