Mtandao wa kudhibiti Malaria Nchini(TANAM) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Chini ya Ufadhili wa Global Fund imekabidhi Jumla ya pikipiki 14 kwa Asasi mbalimbali za kanda ya Kusini ikiwa ni jitihada za
kuelimisha Jamii jinsi ya kupigana na adui malaria ambapo tayari
Asasi hiyo ikiwa tayari imefikisha elimu mpaka ngazi ya Kata ikiwa
pamoja na Utunzaji wa Mazingira.
Pamoja na lengo la serikalila kujenga zahanati katika kila kijiji na
kituo cha afya kwenye kila kata nchi nzima imelezwa kuwa elimu
ikitolewa ya udhibiti wa Ugonjwa huo kwa wananchi itasaidia zaidi
kupunguza ugonjwa huo, kabla ya kujenga zahanati na vituo vya afya
ikiwemo Ugawaji wa Vyandarua.
Akiongea mara Baada ya kukabidhi Pikipiki kwa Asasi za Mkoa wa Lindi na Mtwara pamoja na ya Mratibu wa Mtandao wa kudhibiti Malaria kanda ya Kusini Katika hafla fupi iliyofanyika Leo, Katibu Tawala Msaidizi Huduma za Uchumi Mkoa wa Lindi, Bw John Likango sambamba na kutoa wito kwa Asasi hizo juu ya Matumizi ya Pikipiki hizo alieleza kuwa Udhibiti wa Malaria utafanikiwa ikiwa Elimu itatolewa zaidi kupunguza vyanzo vya Ugonjwa huo hapa Nchini.
Aidha mwakilishi wa Mtandao Huo toka Makao Makuu,Bw Sunny Kuluvia sambamba na kutoa Pikipiki hizo aliwaomba wananchi kutoa Ushirikiano ambapo wakielimishwa kuhusu malaria, watafahamu njia sahihi ya kupambana nayo, ikiwemo kusafisha mazingira ili kuua mazalia ya mbu wanaoambukiza ugonjwa huo hatari kwa jukumu ni lao kushirikiana na Serikali.
Kwa upande wake Katibu wa Asasi ya Lisawe ya Mjini Lindi Bi Prisisca
Unga alieleza jinsi watakavyoshirikiana na Jamii kupitia mawakala wa
Kata kurahisisha utoaji wa elimu baada ya kupewa Usafiri Kupitia Mpango jumla ya pikipiki 55 zimenunuliwa kwa ajili ya kanda Tatu zilizo katika mpango huo Nchini huku tayari pikipiki kwa Asasi 13 za Mkoa wa Lindi na Mtwara zimekabidhiwa ambapo Asasi hizo ni Lisawe
ya Lindi Mjini, Shikwayuki-Kilwa, Ropa-Ruangwa, Mukemba-Mtwara
vijijini, Masha-Mtwara/Mikindani, FEM-Lindi Vijijini,
Naeso-Nachingwea, Lifa-Liwale, Lefe-Nanyumbu, Neda-Newala, Shikum-Masasi na TWA ya Tandahimba zimekabidhiwa ili kusaidia utoaji wa Elimu kwa Jamii.
Tags
HABARI ZA KITAIFA