Amesema Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na kushirikisha vilabu na watu binafsi wenye ujuzi wa kuogelea unaofikia kiwango cha kushiriki mashindano. Aidha Bi. Najat Ahmed ameomba wadau zaidi kujitokeza kudhamini mashindano hayo na kuiomba Serikali ijitokeze na kujenga mabwawa yanayohitajika kwa ajili ya watu kujifunza kuogelea ili kuweza kujiokoa katika ajali za majini.
Official wakijipanga tayari kuanza mashindano hayo yaliyohusisha Clubs mbalimbali kutoka sehemu tofauti.
Pichani juu na chini ni washiriki wajitosa kwenye bwawa hilo kuchuana katika mashindano ya kuogelea yaliyoratibiwa na TALISS Swim Club na kudhaminiwa na kampuni ya CFAO Motors ya jijini Dar.
PICHA KWA HISANI YA MICHUZI JR BLOG
Tags
HABARI ZA KITAIFA