wa Jimbo la Lindi Mjini,Salum Barwany
Na Abdulaziz,Lindi
Jeshi la Polisi Mkoani Lindi limefanikiwa kusitisha maandamano yaliyokuwa yameandaliwa na Chama cha Wananchi CUF Kufanyika jana katika manispaa ya Lindi.
Kusitishwa kwa maandamano hayo kunafuatia barua ya Kamanda wea Polisi
wilaya ya Lindi ya tarehe 20 mwezi huu kwa Chama hicho cha CUF Kuyakataa maombi yao ya kutaka kufanya maandamano makubwa na mkutano wa Hadhara Katika barua hiyo Cuf ilitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi wilaya ya Lindi ya kutaka kufanyika maandamano makubwa na mkutano wa Hadhara kwa lengo la kuishinikiza serikali kutoa tathmini ya Maendeleo ya Miradi ya Gesi asilia,Maji,Stakabadhi ghalani pamoja kupatiwa taarifa ya kuanza kutekelezwa kwa ahadi za serikali juu ya ujenzi wa viwanda vitavyotokana na gesi na kuitafsiri mikataba ya gesi.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na suala
hilo la Maandamano Mbunge wa chama hicho ambae pia ni Mwenyekiti wa Wilaya, Salum Barwany amesema chama chake kimelazimika kusitisha maandamano hayo kwa muda hadi tarehe 03 mwezi ujao na kusisitiza kwamba maandamano ni haki ya Msingi kuwawezesha wananchi kutoa kero zao
Sambamba na hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,George Mwakajinga ameeleza kuwa Ofisi yake imeamua kuzuia maandamano hayo kufuatia Mialiko mbalimbali iliyotolewa kwa mkoa wa Mtwara ambako hivi karibuni kulitokea hali ya uvunjifu wa Amani na kusababisha Vifo, uchomaji wa moto kwa nyumba za wabunge na serikali ikiwemo magari
‘’Maandamano ni haki ya msingi kwa vyama vya siasa ila inatushangaza unapotoa mialiko kwa mikoa mingine hii imetuweka njia panda inakuwaje maandamano ya Lindi waje na Mtwara hii Hapana ni lazima Jeshi lijipange ndio tutaruhusu kwa kuwa tetesi tulizozipata wengine wanakuja kwa ajili ya Fujo..alimalizia Kamanda Mwakajinga.
Tags
HABARI ZA KITAIFA