Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Bi Agness Hokororo akifungua Mafunzo ya siku 2 Kwa Wachimbaji wadogo wilaya ya RuangwaWadau wa Madini wilaya ya Ruangwa wakiwa katika picha ya Pamoja Na Mgeni Rasmi,Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Bi Agness Hokororo.Wadau wa Madini wilaya ya Ruangwa wakisikiliza kwa makini mambo waliyokuwa wakiambia katika mafunzo ya siku mbili yaliyofunguliwa na Mkuu wa wilaya hiyo bi. Agnes Hokororo
Na Abdulaziz,Ruangwa
Wachimbaji wadogowadogo wa madini Wilayani Ruangwa wametakiwa kuacha
kufanya kazi katika mfumo usio rasmi badala yake wabadilike kwa kuingia katika mfumo rasmi ambao utawawezesha kukubalika na taasisi za fedha kutokana na kukua kwa sekta ya Madini Duniani ikiendana na Mabadiliko ya Uchumi hapa Nchini.
Wito huo Umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Iindi,Bi Agness Hokororo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili ya wachimbaji wadogo wa madini katika wilayani humo ambapo alibainisha kuwa uchimbaji mdogo ni sekta ya kibiashara ambayo inaweza kuongeza kipato cha wananchi kwa kuongeza ajira pamoja na uchangia ukuaji wa pato la taifa Licha ya kutokuwepo kwa taarifa sahihi za uzalishaji na uuzaji wa madini na wachimbaji wadogo kutozifanya shughuli za uchimbaji madini kama shughuli maalum ambazo zinaweza kuajiri na kuajiri
Mafunzo hayo ya siku mbili yamewezeshwa na Wizara ya Nishati na Madini na kuratibiwa na ofisi ya Kamishna wa Madini kanda ya kusini na kuhusisisha Wachimbaji wadogo,Madiwani,Watendaji wa vijiji/kata ambapo mada mbali mbali zitatolewa zikiwamao za Sheria ya madini ya mwaka 2010,Ufafanuzi wa sera ya madini,Fursa za madini zilizopo Ruangwa na Matumizi salama ya Baruti ambapo pia watapewa Mwongozo wa kuandaa mpango wa kutunza Mazingira(EPP0)