Unknown Unknown Author
Title: MASASI YACHAFUKA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
WATU Saba akiwemo askari polisi mmoja wameuawa katika vurugu zinazoendelea wilayani Masasi mkoani Mtwara, zikiwazimebebasura ya kupinga ges...

majeruhiWATU Saba akiwemo askari polisi mmoja wameuawa katika vurugu
zinazoendelea wilayani Masasi mkoani Mtwara, zikiwazimebebasura ya kupinga gesi kwenda Dar es Salaam.Muuguzi wa zamu hospitali ya wilaya ya Masasi, Mkomaindo Fatuma Timbu amethibitisha kupokea maiti za watu saba.
Majeruhi ambao idadi yao haijajulikana wamekimbizwa hospitali ya
misheni ya Ndanda kwa matibabu na hali bado ni tete Vurugu kubwa
zilianza majira yasaa 4 asubuhi baada ya polisi waliokuwa wakiendesha pikipiki kumgonga mtu na kukataa kutoa ushirikiano
moto 4Hata hivyo hoja hiyo ilihamia kwenye gesina kundi la viajana mara moja walivamianyumba ya mbunge wa Masasi, Mariam kasembe na kuiwasha moto, pamoja na magari mawili. Aidha vijana hao walivamia nyumba ya Anna Abdallah na kuiteketeza kwa moto, kabla ya kuivania ofisi ya CCM wilaya na kuichoma moto pamoja na magari matatu. Hasira za wananchi hao zilifika kituo kidogo cha polisi kilichopo Mkuti na kukichoma moto, baadae walichoma moto magari matano ya halmashauri ya wilaya.Pia walichoma moto ofisi ya elimu ya halmshauri ya wilaya Masasi vijijini, kabla ya kuichoma ofisi ya maliasili joni hii. Polisi kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya mkoa inadaiwa walitumia risasi za moto na kusababisha vifo vya watu Sita huku polisi akidaiwa kuuawa kwa kupigwa na wananchi….

About Author

Advertisement

 
Top