Na Saleh Ally, Muscat
RAHMA Al Kharusi si jina geni katika mchezo wa soka Tanzania, wengi wanamkumbuka wakati alipoamua kuingia katika kuisaidia Twiga Stars na baadaye akaipeleka nchini Marekani lakini baadaye akapotea.
Akarejea akiwa upande wa African Lyon, akasaidia mambo mengi na kufanya timu hiyo izidi kupata umaarufu, lakini baadaye hakuonekana hadi alipokuja kuibukia Simba na kusema hapo ndiyo nyumbani.
Mfanyabiashara huyo bilionea anasisitiza ametua Simba baada ya kuombwa kukubali uteuzi wa mjumbe wa kamati ya utendaji na anaamini atakuwa mshindani mkubwa wa kuleta maendeleo.Rahma ni Rais wa Makampuni ya RBP Oil ambayo yanafanya biashara mbalimbali katika nchi tofauti za Afrika. Baadhi ya biashara hizo ni uuzaji wa mafuta ya ‘dizeli’ na petrol katika nchi mbalimbali, lakini pia vyakula pamoja na samani za ndani.
Nchi za Afrika ambazo makampuni yake yanafanya kazi ni pamoja na Tanzania, DR Congo, Sudan Kusini na Uganda lakini pia kampuni zake zinafanya biashara katika nchi za Oman na Qatar.
Rahma, maarufu kama Queen of Bees, yaani Malkia wa Nyuki, anataka Simba yenye mabadiliko makubwa huku akitumia msemo wa, “Nikianza jambo, lazima nilimalize.”
Anataka kuiona Simba ikiwa na mambo mengi yenye mabadiliko, lakini anataka timu ya wanawake pamoja na timu imara ya vijana ambayo itaiwezesha Simba kuwa na msingi hapo baadaye.
“Simba walikuja kuniomba, sikuona kama kuna ubaya wa kukubali kuingia. Wakati tunakua nyumbani nilikuwa nikimuona baba yangu akiisaidia Simba, nasi tukajikuta tunaingia Simba. Tangu nikiwa mdogo, hii ndiyo timu yangu.
“Huo ni ushabiki, lakini ninachotaka mimi ni maendeleo. Najua kuna presha kubwa kutoka kwa Yanga, mimi nitaichukulia kama changamoto na nitashindana kuleta maendeleo. Najua Yanga wanaye (Yusuf) Manji, nitashindana naye sana.
“Najua nikishindana na Manji nitaleta maendeleo upande wa Simba, lakini nitapenda uwe ushindani wa kimaendeleo na si zaidi. Kama nitaona ni ushindani wa kutaka kuumizana nitajiweka kando, nataka maendeleo ambayo ndiyo mafanikio.
“Sitaki ugomvi, ndiyo maana utaona nilijiondoa Twiga na African Lyon. Migogoro ni kati ya vitu nisivyopenda kabisa, halafu Manji ni mtu ninayeheshimiana naye sana. Hivyo sitaki malumbano ila ushindani wa kuleta maendeleo.
“Nitashirikiana na wenzangu kuifanyia Simba kila linalowezekana ambalo litaonekana ni kubwa. Safari ya hapa Oman nataka pia iwe ni yenye manufaa. Ndiyo maana niliwaambia wachezaji lazima wajitume na kuonyesha muda wao walioutumia hapa ulikuwa na manufaa.
HABARI HII KWA HISANI YA GPL: INAENDELEA BOFYA HAPA
MALKIA WA NYUKI: NITASHINDANA NA MANJI
Title: MALKIA WA NYUKI: NITASHINDANA NA MANJI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Saleh Ally, Muscat RAHMA Al Kharusi si jina geni katika mchezo wa soka Tanzania, wengi wanamkumbuka wakati alipoamua kuingia katika kuisa...