Makundi ya upinzani ya Kuwait yamesema hatua yao ya kuususia uchaguzi wa wabunge imefaulu, baada ya matokeo rasmi kuonesha kuwa idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ni ndogo.
Wizara ya habari imesema asilimia 39 tu ya wapigaji kura, kati ya watu 420,000 waliokuwa na haki ya kura, ndio walioshiriki; ikilinganishwa na karibu asilimia 60 mwezi wa Februari.
Upinzani - wenye msimamo wa kidini na wastani - haukugombea viti ili kulalamika juu ya mabadiliko ya kanuni za kupiga kura, ambayo ulisema unaonea upinzani.
Mvutano kati ya wabunge na mawaziri - wengi kutoka ukoo wa mfalme - umezidi mwaka huu.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.