Unknown Unknown Author
Title: SIMBA SC YASISTIZA MUDDE NI MCHEZAJI WAKE HALALI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SIMBA SC imesema kwamba Mussa Mudde ni miongoni mwa wachezaji wake wa kigeni wanne ilionao kwa sasa na imeshangazwa sana na habari zilizoand...
SIMBA SC imesema kwamba Mussa Mudde ni miongoni mwa wachezaji wake wa kigeni wanne ilionao kwa sasa na imeshangazwa sana na habari zilizoandikwa katika tovuti ya supersport.com ya Afrika Kusini zikisema kwamba anarejea Sofapaka.
Akizungumza kwa simu jana kutoka Uingereza, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba Mudde ana mkataba wa miaka miwili na Wekundu hao wa Msimbazi.
“Nashangaa hizo habari wamezitoa wapi, huyu ni mchezaji wetu na mimi nilipoondoka Dar es Salaam nilimuacha pale, ni vema wakati mwingine wakawa wanawasiliana na sisi pia kutuuliza,”alisema Hans Poppe.
Wiki hii, supersport.com imeandika kwamba Mudde anarejea Sofapaka baada ya kuona mambo hayamuendei vizuri Simba SC.
Tovuti hiyo ilimnukuu na rais wa Sofapaka, Elly Kalekwa ambaye alisema kwamba ameingia mkataba wa miaka miwili na kiungo huyo mkabaji wa Mganda arejee Nairobi.
Mbali na Mudde, wachezaji wengine wa kigeni ambao hadi sasa wana uhakika wa kuvaa jezi za Simba SC ni kipa Abbel Dhaira, mshambuliaji Emmanuel Okwi wote kutoka Uganda pia na beki Komalbil Keita kutoka Mali.

Kutoka kikosi cha Simba kilichocheza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, wachezaji Felix Sunzu kutoka Zambia, Daniel Akuffo kutoka Ghana na beki Paschal Ochieng kutoka Kenya, wametupiwa virago.
Mudde alisajiliwa tangu mwanzo wa msimu, lakini akaenguliwa kutokana na kuwa majeruhi na hakucheza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, wakati Dhaira pia amesajiliwa wiki iliyopita ili kuanza kazi Januari.






About Author

Advertisement

 
Top