MUNGU AKINIJALIA HADI MWAKANI NATAKA NIWAINUE UNDERGROUND KUMI WAWE MASTAA!

Msanii nyota wa filamu Tanzania Nisha amesema kuwa ana mpango maalum wa kuwainua wasanii kumi wachanga na kuwa mastaa kabisa kwa vile wamekuwa wakisahaulika sana na kukumbwa na mitihani mizito.

Nisha  alisema kuwa"Wasanii wachanga wanateseka sana wengi wao hasa wakike wanakumbwa na mitihani ya rushwa ya ngono bila msaada wowote nitawasaidia kadri nitakavyojaliwa kwani wako wengi wana vipaji" Alisema Nisha

Msanii huyo aliongeza kusema kuwa kama Mungu amemjalia yeye kupiga hatua kadhaa mbele lazima na yeye awavute wengine na sio kuwa wachoyo kwani hata kanuni za vitabu vya mungu vinasema ukitaka kufanikiwa kwa jambo lolote usiwe mchoyo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post