Unknown Unknown Author
Title: CAF KUFANYA UKAGUZI WA ‘LESENI ZA KLABU’ JANUARI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litatuma ofisa wake nchini mwezi ujao kwa ajili ya kufanya ukaguzi kwenye klabu za Ligi Kuu ya Tan...
TFF_LOGOShirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litatuma ofisa wake nchini mwezi ujao kwa ajili ya kufanya ukaguzi kwenye klabu za Ligi Kuu ya Tanzania kabla ya kutoa leseni kwa zile ambazo zitakuwa zimekidhi vigezo vilivyowekwa. Ili klabu ishiriki mashindano ya CAF ni lazima iwe na leseni hiyo.
Kwa mujibu wa CAF, ofisa huyo atakuwa nchini kuanzia Januari 7 mwakani ambapo atafanya ukaguzi huo hadi Januari 14 mwakani. Mbali ya ukaguzi katika klabu, pia ofisa huyo atakagua viwanja vitakavyotumika katika mashindano yake na hoteli ambazo timu kutoka nje zitakuwa zinafikia kabla ya mechi.

Baadhi ya masharti kabla ya klabu kupewa leseni ya CAF ni pamoja na kuwa na ofisi (physical address), uwanja wake wa mazoezi, programu ya maendeleo kwa vijana, sekretarieti ya kuajiriwa, hesabu za fedha zilizokaguliwa (audited accounts) na benchi la ufundi linaloundwa na watu wenye sifa zinazostahili.

Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)



About Author

Advertisement

 
Top