Unknown Unknown Author
Title: LIGI KUU ENGLAND WEEKEND HII DEC.15/2012
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
LIGI KUU ENGLAND inaendelea Jumamosi kwa Mabingwa watetezi Manchester City kusafiri kwenda St James Park kuivaa Newcastle ikiwa ni Mechi ya...
BPL_LOGO
LIGI KUU ENGLAND inaendelea Jumamosi kwa Mabingwa watetezi Manchester City kusafiri kwenda St James Park kuivaa Newcastle ikiwa ni Mechi yao ya kwanza tangu wapewe kipigo chao cha kwanza Msimu huu kwenye Ligi walipofungwa na Manchester United Bao 3-2 Uwanjani Etihad na Wababe Man United, baadae Siku hiyo hiyo, wao watakuwa nyumbani kucheza na Sunderland.
ZIFUATAZO NI DONDOO FUPI KUHUSU MECHI ZA WIKIENDI:
RATIBA:                  Jumamosi 15 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Newcastle v Man City
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Aston Villa
Man United v Sunderland
Norwich v Wigan
QPR v Fulham
Stoke v Everton
+++++++++++++++++++
Newcastle v Man City
Man City wanaingia kwenye Mechi hii wakiwa wametoka kupokea kipigo chao cha kwanza Msimu huu mikononi mwa Man United ambao ndio wapo kileleni na Man City kubakia nafasi ya pili Pointi 6 nyuma yao.
Lakini Man City wanakutana na Newcastle, Timu ambayo imefungwa Mechi 5 kati ya 6 za Ligi walizocheza mwishoni lakini tatizo hili hasa ni kukabiliwa na majeruhi kibao.
Kwa upande wa Man City, Wadau wengi huwa wanajiuliza ni kwa sababu gani Meneja wao huwa anampiga benchi Carlos Tevez na kumuanzisha Mario Balotelli ambae, mara nyingi, hucheza chini ya kiwango kama alivyoonyesha Jumapili iliyopita walivyochapwa 3-2 na Man United.
Liverpool v Aston Villa
Liverpool wameanza kuzinduka hasa baada ya kuichapa West Ham Mechi iliyopita walipocheza bila ya Mfungaji wao Luis Suarez aliekuwa kifungoni lakini kwenye Mechi hii na Aston Villa Suarez atarudi dimbani.
Aston Villa, baada ya kupata ushindi mnono wa Bao 4-1 hapo juzi walipoifunga Norwich City na kutinga Nusu Fainali ya CAPITAL ONE CUP, wataingia kwenye Mechi hii wakiwa na morali kubwa.
Man Unted v Sunderland
Sunderland walipata ushindi muhimu Jumanne iliyopita walipoitwanga Bao 3-0 Reading lakini Jumamosi  wanapambana na Vinara wa Ligi, Manchester United, ambao Jumapili iliyopita walipata ushindi mtamu wa ugenini walipowatwanga Mahasimu wao Man City Bao 3-2 na kuwapa kipigo chao cha kwanza Msimu huu na pia kuvunja rekodi ya City kutofungwa kwao Etihad kwa Miaka miwili.
Pia, Man United wana habari njema za kurudi Uwanjani kwa Nahodha wao Nemanja Vidic ambae alikuwa nje tangu Septemba 19 akiuguza goti lake.

Norwich v Wigan
Norwich watataka kufuta machungu ya kutwangwa Bao 4-1 wakiwa Uwanja huu huu wa nyumbani, Carrow Road, walipopigwa 4-1 na Aston Villa na kutolewa nje ya CAPITAL ONE CUP.
Lakini, Norwich wanakutana na Wigan isiyotabirika na lolote linaweza kutokea.
QPR v Fulham
Je hii itakuwa ni Mechi ambayo QPR watapata ushindi wao wa kwanza kwenye Ligi Msimu huu?
Tangu Meneja mpya Harry Redknapp aanze kuiongoza QPR wamecheza Mechi 3 na hawajafungwa na zipo kila dalili sasa wanacheza Kitimu kupita ilivyokuwa chini ya Meneja aliepita Mark Hughes.
Lakini, Fulham, ambao Jumatatu waliifunga Newcastle na kusimamisha wimbi lao la kufungwa mfululizo, si Timu rahisi.
Stoke v Everton
Stoke City ni wagumu na nguvu kazi wakicheza kwao lakini Everton, kama walivyoonyesha Wiki iliyopita walipopindua kuwa nyuma Bao 1-0 walipokuwa ugenini White Hart Lane na kuichapa Tottenham Bao 2-1 katika Dakika za majeruhi, ni Timu hatari.
Hii ni Mechi ngumu kuitabiri.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:                    Jumapili 16 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Tottenham v  Swansea
[SAA 1 Usiku]
West Brom v West Ham
+++++++++++++++++++++++
Tottenham v Swansea
Hii ni gemu ambayo lazima Tottenham washinde ikiwa kweli wanataka kumaliza Ligi wakiwa 4 bora hasa kwa vile Swansea City sio Timu yenye msimamo thabiti na huwa haitabiriki kama vile walivyofanya kwa kwenda ugenini na kuifunga Arsenal lakini waliporudi nyumbani Mechi iliyofuata wakachapwa na Norwich City.
West Brom v West Ham
West Brom wamefungwa Mechi 3 mfululizo hadi sasa lakini kipigo chao cha mwisho mikononi mwa Arsenal kilichangiwa na Arsenal kupewa Penati isiyostahili.
Wapinzani wa WBA ni West Ham ambao huwa ubwete kwa Mechi za ugenini ingawa katika Mechi zao za hivi karibuni wapinzani wao walikuwa baadhi ya Vigogo kama vile Spurs, Manchester United, Chelsea na Liverpool.
Hii ni Mechi tamu na yeyote anaweza kushinda.
Prediction: 2-1
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:                  Jumatatu 17 Desemba 2012
[SAA 5 Usiku]
Reading v Arsenal
+++++++++++++++++++++++
Reading v Arsenal
Hii si Bigi Mechi lakini kwa Wadau wa Arsenal kwao ni Mechi muhimu mno hasa baada ya juzi kutupwa nje ya CAPITAL ONE CUP na Timu ya Daraja la 4 Bradford City na kuibua hali tete Klabuni kwao ikiwakumbusha sasa ni Miaka 8 tangu watwae Taji lolote.
Mara ya mwisho kukutana kwa Timu hizi, Arsenal walishinda Bao 7-5 kwenye CAPITAL ONE CUP.
+++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:  [Kila Timu Mechi 16]
1 Man United Pointi 39
2 Man City 33
3 Chelsea 29
4 Everton 26
===============
5 Tottenham 26
6 WBA 26
7 Arsenal 24
8 Swansea 23
9 Stoke 23
10 Liverpool 22
11 West Ham 22
12 Norwich 22
13 Fulham 20
14 Newcastle 17
15 Sunderland 16
16 Southampton 15
17 Aston Villa 15
===============
18 Wigan 15
19 Readind 9
20 QPR 7












































































About Author

Advertisement

 
Top