BERENIKI KIMIRO NDIO MSHINDI WA MAISHA PLUS S3.

maisha plus villageMshindi wa Maisha Plus 2012 ni BERENIKI KIMIRO, amejishidia Tshs. Millioni 20, -- Mshindi wa Pili ni Venance Mushi amejishindia Tshs. Million 6…. Mshindi wa Tatu ni Justine Bayo, amejishindia Tshs. Million 4.

Mshindi wa Maisha Plus 2012, BERENIKI KIMIRO ameanza kwa Kumshukuru Mungu kwa ushindi, asema ye si kitu kwa wenzake, hilo ni zali tu.. Amemshukuru baba yake mzazi kwa kumshauri kusali.. Amewashukuru pia wapenzi watazamaji kwa kumpiga kura, ameahidi kuendeleza kile alichokianza kijijini na kuitendea haki nchi yake.. Amemshukuru babu, Brother Masoud na Crew nzima ya Maisha Plus.. Amemshukuru pia mwanae Kelvin (6yrs) kwa kuvumilia kipindi chote bila kuongea na mama.. Amesema Mungu amejibu maombi yake kwani ukipiga goti, maombi yako yatajibiwa..

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post