Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa ameiambia Mahakama ya
Mbeya kuwa upelelezi wa kesi ya mtuhumiwa Wilvina Mkandala ,24,
umekamilika na akaomba tarehe ya kuanza kusikilizwa kesi hiyo ambapo
inadaiwa alisababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo imemsababishia
ulemavu mtoto Aneth (3) ambaye amekatwa mkono.
Alisema upande wa Jamhuri una mashahidi wanne ambao wataanza kutoa ushahidi wao mahakamani hapo Novemba 22, mwaka huu kutokana na upelelezi kukamilika na akawataja kuwa ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Shukuru Mwakanyamale, dokta Paul anayemtibu mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, polisi aliyepeleleza kesi hiyo, WP Pudensia na Habiba Mwakanyamale ambao wako tayari kufika mahakamani na kutoa ushahidi wao.
Mulisa akisoma mashtaka mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo, Gilbert Ndeuruo amesema kosa alilolifanya ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu cha 222(a) sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2002.
Mshtakiwa amekana shitaka hilo ambapo ametupwa rumande hadi Novemba 22, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.