Chelsea wiki hii ina kibarua kigumu, mbali tu na kuangazia mechi dhidi ya Shakhtar Donetsk na Liverpool.
Wachezaji, makocha na pia wafanyakazi wa klabu hiyo ya London, huenda wakawapokea maafisa kutoka chama cha soka cha FA, na vilevile wale wa idara ya polisi ya Metropolitan.
Wote watakuwa na nia ya kuthibitisha yaliyotamkwa na mwamuzi Mark Clattenburg, au kutosemwa, wakati timu ya Chelsea ikiwa uwanja wa nyumbani, na maarufu kwa jina The Blues, iliposhindwa na Manchester United, katika uwanja wa Stamford Bridge, tarehe 28 Oktoba.
Mazungumzo kati ya wahusika wote yataamua kama Clattenburg atashtakiwa kwa kutumia lugha isiyofaa, dhidi ya mchezaji wa kimataifa wa Nigeria, Jon Obi Mikel, ambaye ni kiungo cha kati wa timu ya Chelsea.
Huku chama cha FA kikikabiliwa na shinikizo za kuepuka kesi iliyochukua muda mrefu kupata suluhu kumhusu John Terry, nia ni kuthibitisha kwamba shahidi wa mwisho katika kesi ya hivi sasa, Clattenburg, atahojiwa kwa haraka kabla ya mwisho wa wiki.
Tayari Clattenburg ameshafanya mashauri na chama cha waamuzi wataalamu, ili kurudi kazini mwishoni mwa wiki.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.