Unknown Unknown Author
Title: Mikoa Ya Lindi Na Mtwara Yapata Umeme Wa Uhakika
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mikoa Ya Lindi Na Mtwara Yapata Umeme Wa Uhakika Na Veronica Kazimoto – MAELEZO Mtwara 3 Oktoba, 2012. Serikali imeboresha miundombinu ya ...

Mikoa Ya Lindi Na Mtwara Yapata Umeme Wa Uhakika Na Veronica Kazimoto – MAELEZO Mtwara 3 Oktoba, 2012.
Serikali imeboresha miundombinu ya umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na wilaya zake kwa kuwa na mtambo unaozalisha umeme mwingi kuzidi mahitaji ya mikoa hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme TANESCO Mkoa wa Mtwara Mhandisi Daniel Kiando alisema kwa sasa mtambo una uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati kumi na nane (18) wakati mahitaji ya mikoa hiyo ni megawati kumi na tatu (13).
“Kwa sasa mtambo wetu unazalisha umeme wa kutosha kiasi kwamba tuna ziada ya umeme wa megawati tano, hata hivyo tunaendelea kuzalisha umeme kulingana na mahitaji ya mikoa yetu,” alisema Kiando. Kiando amefafanua kuwa mtambo huo unaozalisha umeme kwa kutumia gesi unasambaza umeme wa megawati 7.5 katika Mkoa wa Mtwara na megawati 5.5 katika Mkoa wa Lindi.


Kutokana na uboreshaji huo, wananchi wa Mtwara na Lindi wamepata punguzo la umeme ambapo kwa sasa wanalipia umeme kwa elfu tisini na tisa badala ya laki nne na elfu hamsini na tano na mwisho wa punguzo hili ni mwezi Desemba mwaka huu.
Mwezi Aprili mwaka huu, Serikali iliamua kuchukua mtambo huo wa kuzalisha umeme kutoka kwa wawekezaji wa Artmas na hivi sasa mtambo unazalisha umeme kwa kutumia gesi badala ya mafuta mazito kama ilivyokuwa hapo awali.

About Author

Advertisement

 
Top