Unknown Unknown Author
Title: Washiriki Redds Miss Tanzania 2012 kuingia kambini Oktoba 2, Fainali kufanyika Novemba 3
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa wa Shindano kubwa la Urembo la Redd’s Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) akiz...
Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa wa Shindano kubwa la Urembo la Redd’s Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo juu ya kuanza rasmi kwa kambi ya Miss Tanzania 2012 pamoja na siku ya fainali ya Shindano hilo. Kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Redd’s, Victoria Kimaro na Kulia ni Miss Tanzania 2011, Salha IzraelMkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa wa Shindano kubwa la Urembo la Redd’s Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo juu ya Mashindano ya Redds Miss Tanzania . Katikati ni Meneja wa Kinywaji cha Redd’s Original , Victoria Kimaro na Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye.Miss Tanzania 2011, Salha Izrael (kushoto) akiwa na Mmoja wa washiriki wa Shindano Miss Tanzania 2011, Jennifer Kakolaki.Waandishi wa Kongwe wa Habari za Urembo, michezo na burudani, katika magazeti kutoka kulia ni Somoe Ng’itu wa Nipashe, Asha Kigundula wa JamboLeo na Mwani Nyangasa wa Mtanzania/Dimba na Bingwa wakimsikiliza kwa makini Hashim Lundenga.


Mashindano ya Redds Miss Tanzania kwa sasa yamekamilika katika hatua zote na hatua ya mwisho ilikuwa hatua ya kanda ambayo kwa sasa imekamilika na kufanikiwa kuwapata warembo jumla ya 30 .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa LINO INTERNATIONAL AGENCY, Hashim Lundenga alisema mashindano kiujumla katika ngazi zote hadi kanda yamekuwa na mafanikio makubwa na kuonyesha kuwa fainali ya Taifa ya mwaka huu itakuwa na ushindani wa hali ya Juu.
Washiriki wengi wa mwaka huu kwa asilmia 90 ni wasomi wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wengine wanatarajia kujiunga na Vyuo Vikuu, jambo ambalo litaleta hamasa kubwa katika shindano la mwaka huu. 
Baada ya kukamilika kwa mashindano hayo ya Kanda kwa sasa tunatangaza rasmi kuwa warembo wote 30 walioshinda na kuingia katika kinyang,anyiro cha Redds Miss Tanzania 2012 wataingia kambini siku ya jumanne October 2,2012 katika Hotel yenye hadhi ya kimataifa ya GIRAFFE HOTEL Iliyopo hapa Jijini Dar Es salaam,Washiriki hao watakuwa kambini kwa muda wa mwezi mmoja. 
Tunapenda kuwajulisha wadau wa tasnia ya urembo kwamba shindano la REDDS MISS TANZANIA 2012 litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 03 November 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Peal (Ubungo Plaza). 
Kwa Upande wake Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro alisema wao kama wadhamini wakuu wa Redds Miss Tanzania wamejipanga kwa nguvu kubwa kutoa burudani ya aina yake kwa wadau wote wa tasnia ya urembo hapa nchini sambamba na kuhakikisha warembo wote waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali.
Kwa kuzingatia mabadiliko ya Kalenda ya Mashindano ya urembo ya Dunia, Mrembo wa Tanzania atakuwa na muda mrefu wa maandalizi kwani atatakiwa kuripoti katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia katikati ya mwaka ujao. 2013.

About Author

Advertisement

 
Top