Unknown Unknown Author
Title: STR8MUZIK Free Style 2012 zang’ara Mwanza
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mshindi wa mpambano wa ma-DJ wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani mwanza DJ Juma Ramadhani(Kati) akifanya vitu vyake mara baada ya kukabidhiw...

Mshindi wa mpambano wa ma-DJ wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani mwanza DJ Juma Ramadhani(Kati) akifanya vitu vyake mara baada ya kukabidhiwa chombo cha kupigishia muziki chenye thmani ya Sh mil 7 na Meneja wa TCC Mkoa wa Mwanza Deogratius Kamugisha(Kulia), huku mshindi wa upande wa ma-MC mkoani humo Joash Magadula akishuhudia na zawadi yake mkononi.Mmoja wa wanakundi cha waburudishaji cha BFB cha mkoani Mwanza akifanya vitu vyake katika mpambano wa kusaka ma-MCs na DJs wa STR8MUZIK Freestyle 2012 mkoani mwanza uliofanyika katika ukumbi wa Stone mjini humo jana usiku.
Meneja wa TCC Mkoani Mwanza Deogratius Kamugisha akimkabishi tuzo MC bora wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani Mwanza Joash Magadula katika mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Stone mjini humo jana.Mashabiki wa ST8MUZIK Freestyle 2012 mkoani Mwanza wakiwa wamembeba juu MC bora wa mwaka mkoani humo Joash Magadula katika mpambano uliofanyika jana usiku katika ukumbi wa Stone mjini humo.Meneja wa TCC tawi la Mwanza, Bw Deogratius Kamugisha (Katikati) akipozi na washindi wa mpambano wa ma MCs na DJs STR8MUZIK Freetyle 2012 mkoani mwanza. Kutoka kushoto ni Mshindi wa pili wa DJs Ruyobya Johannes a.k.a DJ Yt,Mshindi wa kwanza kwa DJs Juma Ramadhani,Msindi wa Pili katika kategori ya ma-MCs Nchana Antony na Mshindi wa MCs Joash Magadula a.k.a MC Magadash.

About Author

Advertisement

 
Top