Unknown Unknown Author
Title: Rais Kikwete Ziarani Nchini Kenya
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya pamoja na ujumbe wa...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya pamoja na ujumbe wake wakiingia Ikulu ya Nairobi Jumanne, 11 Septemba , 2012, alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Waziri wa Elimu ya Juu wa Kenya, Mheshimiwa Margaret Kamar alipowasili Chuo Kikuu cha Kenyatta kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo hicho.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu ya Juu, Mheshimiwa Margaret Kamar na kuhsoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Olive Mugendi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi baada ya kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na wanafunzi wawili waliotoa burudani ya vichekesho wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha KenyattaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na Rais Mwai E. Kibaki, Waziri Mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga (kushoto) na Makamu wa Rais wa Kenya Mhe Kalonzo Musyoka kabla ya Dhifa ya Kitaifa waliyoandaliwa na mwenyeji wao.Rais Mwai E. Kibaki akiongea wakati wa Dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika hoteli ya Inter Continental.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na ujumbe wake na wenyeji wao wakianza Mazungumzo Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na ujumbe wake na wenyeji wakiongea na wanahabari na kisha kupiga picha ya pamoja baada ya Mazungumzo yao Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.
PICHA NA IKULU.

About Author

Advertisement

 
Top