NIJUZE NIJUZE Author
Title: HII NDIO KAULI YA UTPC KUFUATIA KIFO CHA MWANAHABARI MAREHEMU DAUDI MWANGOSI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Wajumbe wa Mkutano Mkuu UTPC wakiwa wamesimama kwa dakika mija kumuombea Marehemu Daudi Mwangosi aliefariki katika Vurugu za Chade...
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=f291359ed0&view=att&th=1399b3825de8caf8&attid=0.1&disp=inline&realattid=file0&safe=1&zw&saduie=AG9B_P9h2yIbIK4rWbHMpyuL8mkP&sadet=1346939243652&sads=OO3RNDYskyM9pEzHaTydi6TqXKI&sadssc=1


Wajumbe wa Mkutano Mkuu UTPC wakiwa wamesimama kwa dakika mija kumuombea Marehemu Daudi Mwangosi aliefariki katika Vurugu za Chadema na Polisi mkoani Iringa
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=f291359ed0&view=att&th=1399b3825de8caf8&attid=0.2&disp=inline&realattid=file2&safe=1&zw&saduie=AG9B_P9h2yIbIK4rWbHMpyuL8mkP&sadet=1346939520859&sads=1XChlbbNfGVU6AsL34lE1I4FI0w 
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi ambae pia ni mwakilishi wa blog hii Mkoani Humo akiwa na Katibu Muhtasi wa Utpc Muda Mfupi kabla ya kuanza kwa Mafunzo ya Uongozi na
Utawala kwa Viongozi wa klabu za Waandishi wa Habari
 https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=f291359ed0&view=att&th=1399b3825de8caf8&attid=0.4&disp=inline&realattid=file4&safe=1&zw&saduie=AG9B_P9h2yIbIK4rWbHMpyuL8mkP&sadet=1346940115959&sads=Vu0Cg_5WxEJ1T8atICBnXYNuD10
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTPC ambao muda wao wa kuwa katika bodi Hiyo Umemalizika na watajiuzulu rasmi kesho
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=f291359ed0&view=att&th=1399b3825de8caf8&attid=0.3&disp=inline&realattid=file3&safe=1&zw&saduie=AG9B_P9h2yIbIK4rWbHMpyuL8mkP&sadet=1346940426409&sads=cfIAdNzUwZbZzcDW3-2kAVYNiHs 
Rais wa kwanza wa UTPC,Bw Ulimboka Mwakiriri(katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Tanga Press Club,Hassan Hashim Na Mjumbe wa Mbeya Press Club,Bi Esther Macha wakibadilishana mawazo nje ya Ukumbi wa Lion Hotel

Picha na Habari...Abdulaziz video

Esther Macha  Na Mwajabu Kigaza

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=f291359ed0&view=att&th=1399b3825de8caf8&attid=0.5&disp=inline&realattid=file5&safe=1&zw&authuser=0&sadnir=2&saduie=AG9B_P9h2yIbIK4rWbHMpyuL8mkP&sadet=1346940636434&sads=SPKSo-ejgiAWDiCxxacgaSEHTsgUMOJA wa Vilabu  vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)umesema kuwa kufuatia mauaji  ya mwandishi wa habari wa Wa kituo cha Channel Ten Mkoani Iringa Bw. Daudi Mwangosi  kimeitaka serikali kuwasimamisha kazi askari waliohusika katika tukio la mauaji ya kinyama ya mwandishi huyo.
Umoja huo umesema kuwa askari walioshiriki katika oparesheni  hiyo ambayo ni haramu kusimamishwa mara moja ili kupisha uchunguzi kufanyika.
Hayo yalisemwa jana  Jijini Dar Es Salaam na  Rais wa UTPC  Bw.Keneth Simbaya wakati alipokuwa akitoa tamko Kwa Viongozi wa Vilabu Mikoani kuhusiana na mauaji  dhidi ya mwandishi wa habari Huyo aliyeuwawa akiwa mikononi mwa polisi katika kijiji cha Nyololo Wilayani Mufindi.
“Hapa tunataka uchunguzi  huu ukikamilika tunaitaka serikali kuutangazia umma na kupisha sheria kwa wale watakaobainika  kuhusika kwa uzembe huo kwa namna moja au nyingine wachukuliwe hatua dhidi ya
mauaji hayo ya  mwandishi wa habari Bw. Daudi Mwangosi”alisema.
Hata hivyo Bw. Simbaya alisema wakati uchunguzi ukiwa unaendelea serikali  iridhie  na kurasimisha  malipo  kwa ajili ya Mjane wa mwandishi huyo  na watoto walioachwa na marehemu ili waweze kujikimu. Aidha alisema licha ya kutoa tamko hilo wanaendelea  kulitazamia jeshi la polisi  kama mdau  mwenye shaka  kwa namna wanavyotenda kazi  zao na  waandishi wa habari  mikoani  na kwamba watataarifu umma kuhusu
mwenendo wao hapo baadae.
“Lakini pia katika mkutano huu tumeridhia  kushirikiana na taasisi zingine za haki za binadamu  ,uwakili na Utetezi ili kubaini  namna bora ya kuishitaki serikali kama mwenendo wa suala hili  hautakuwa unaleta tija Kutokana na vithibitisho  hivyo tunakaribisha mashirika ya haki za binadamu ,asasi zisizokuwa za kiserikali ili kuweza kufanikisha azma hii”alisema Bw. Simbaya.
Akizungumzia kuhusu usalama kwa waandishi wa habari Bw. Simbaya alisema katika kuhakikisha kuwa waandishi wa habari wanafanya kazi yao kwa usalama amelitaka jeshi la polisi  kutoa utaratibu ambao
utawezesha wanahabari  nchini  kufanya kazi kwa usalama bila hofu wala dharau,kutoa elimu kwa jeshi la polisi  kuhusu  umuhimu wa wanahabari na jukumu lao katika Taifa.
Hata  hivyo baadhi ya viongozi wa Vyama vya waandishi wa habari Tanzania  ambao wanahudhulio mkutano mkuu wa  UTPC walisema tamko hilo halijapewa uzito kutokana na tukio la mauaji lenyewe  na jinsi lilivyo
 huku wakitaka  Tamko hilo kupewa uzito wa kina.
“Hili Tamko lilitakiwa kupewa uzito sana kwani  sisi tuliokuwepo katika msiba huo kwa ujumla inasikitisha sana hivyo tamko ni muhimu lipewe uzito zaidi kulingana na mauaji yenyewe yanavyotisha  hivyo tufuate maamuzi ya viongozi wa clabu waliotoa matamko ya kususia habari za polisi mpaka pale watakapokuwa wameridhia  kukaa meza moja na wanahabari  juu ya mauaji hayo”alisema mmoja wa viongozi wa clabu
za waandishi wa habari Tanzania Bw. Christopher Nyenyembe.

About Author

Advertisement

 
Top