HII NDIO KAULI YA SAGNA KUHUSU CLUB YA ARSENAL

Mchezaji wa Arsenal Bacary Sagna amekubali kwamba yuko tayari kuongea na club yake ili kuongeza mkataba lakini bado haelewi kwa nini club hiyo imemuuza mtu kama Alex Song.

Sagna mwenye miaka 29 ya pumzi akiwa anakaribia kurudi kwenye nyasi baada ya kujeruhiwa msimu uliopita amekiri kwamba ana hofu ya maisha ya club yake ya arsenal na sasa ni wazi anatarajia kila msimu arsenal itakua inauza wachezaji.

Kuhusu Van Persie kuuzwa, Sagna anasema alitarajia kabisa kwa sababu ilishajulikana na wachezaji wengi wa Arsenal ni kama kuna kitu kilikua kinaendelea lakini kitu ambacho Sagna hakukitegemea ni kuuzwa kwa Alex Song, ilikua surprise kwa sababu alikua na miaka mitatu imebaki kwenye mkataba wake, hapo Sagna anasisitiza kwamba haelewi kwa nini imetokea kwa song na ni hasara kubwa kwa club.

Namkariri akisema “inapotokea wachezaji wawili waliofanya vizuri msimu uliopita wanaondoka, ni lazima kuwe na maswali mengi, wakati mwingine mtaani nakutana na mashabiki wanaongea na mimi, naelewa wamekasirika, mimi pia nimekasirika”

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post