Unknown Unknown Author
Title: Fainali za Mchezo wa Safari Pool Ufunguzi wafanyika jijini Mwanza
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na wachezaji wa Pool (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Safa...
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na wachezaji wa Pool (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyofunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza katika Hoteli ya Monarch jijini Mwanza jana.Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza akizungumza na wachezaji (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool Taifa katika Hoteli ya Monarch jijini Mwanza.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Fred Mushi. Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza (wapili kulia) akifungua rasmi mashindano ya Safari Pool Taifa .Kulia ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ilemela(OCD),Debora Magiligimba.Wengine kutoka kushoto ni Katibu wa chama cha Pool Mkoa wa Ilala, Mohamed Mwarabu, Mwenyekiti wa kamati ya mashindano, Haji Kapulila na Makamu mwenyekiti wa TAPA, Fred Mushi.Waamuzi wa mchezo wa Pool wakiongoza maandamano ya kuingia ukumbini wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyofunguliwa rasmi jana katika Hoteli ya Monarch jijini Mwanza na Mkuu wa Wilya ya Ilemela, Amina Masenza.

MKUU wa Wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza, Amina Masenza amewataka viongozi wa  vyama vya mchezo wa pool kuanzia Wilaya, Mikoa na Taifa kuwapa nafasi wachezaji wanawake ili kuweza kuwajengea uwezo wa kujiamini wa kucheza mchezo huo.


Masenza aliyasema hayo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa fainali za taifa za mashindano ya 'Safari Lager National Pool Championship 2012', kwenye ukumbi wa hoteli  ya Monarch mkoani hapa.


Alisema kuwa kama viongozi wa vyama vya mchezo huo kuanzia wilaya hadi taifa  watatoa kipaumbele kwa wachezaji wanawake katika kucheza mchezo huo itawasaidia zaidi katika kuwajengea uwezo wa kujiamini na pia itakuwa ni changamoto kwa wanawake wengine kujitokeza.


"Mwanamke akiwezeshwa anaweza, hivyo toeni kipaumbele kwa wachezaji wanawake ili kuweza kuwajengea uwezo wa kujiamini katika kucheza na pia iwe changamoto kwa wanawake wengine kujitokeza zaidi katika kucheza mchezo huu"alisema Masenza.


Aliongeza kwa kuwataka waamuziwatakaochezesha fainali hizo kuchezesha kwa haki ili kuepukana na vurugu zinazoweza kutokea kutokana na uamuzi wa upendeleo.


Masenza alisema kuwa waamuzi kama watachezesha kwa haki ana imani fainali hizo zitamalizika bila vurugu zozote.


"Niwaombe waamuzi chezesheni kwa haki ili kuepuka vurugu ambazo zinaweza kutokea kutokana na maamuzi ambayo siyo mazuri,"alisema.


Aidha amewataka viongozi, wachezaji na mashabiki kuwa na imani na viongozi wao wa taifa   wa  mchezo huo na kuepuka maneno ya pembeni ambayo yanaweza kupelekea vurugu sizokuwa na msingi.


Masenza aliwapongeza wadhamini wakuu wa mchezo huo nchini, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager kwa kuweza kuinua na kuukuza mchezo huo.


Naye meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema kuwa wataendelea kudhamini mchezo huo lengo likiwa ni kuuendeleza na kutoa mchango wao katika jamii kwa faida  wanayoipata kupitia kwenye bia yao.


"Nia ya kuanza kudhamini mchezo wa pool ilikuwa ni kuinua na kuukuza, hivyo tutaendelea kuudhamini huku tukiwa tunatoa pia mchango wetu katika jamii katika faida kidogo tunayopata kupitia kiwenye bbia bia yetu ya Safari Lager,"alisema Shelukindo.


Mkuu wa wilaya ya kipolisi ya Ilemela (OCD),Debora Magiligimba  amewataka viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu zote za mikoa 16 inayoshiriki fainali  hizo kuishi kwa amani katika siku zote za mashindano hayo kutokana na kwamba ulinzi utaimalishwa  na atakayesababisha vurugu atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.


Timu zinazoshiriki fainali hizo na mikoa zinakotoka ikiwa kwenye mabano ni Spider (Tanga), Janja (Manyara), New Stand (Shinyanga), Texas (Tabora), Sabasaba (Lindi), Anatory (Morogoro), Atlantic (Dodoma), Nginja (Iringa) na Blue House (Mbeya).


Nyingine ni Bilele (Kagera), Meeda (Kinondoni), Mbosho (Kilimanjaro), 2eyes (Arusha),Kayumba (Ilala), Sun City (Temeke) na wenyeji Paseansi (Mwanza).


Bingwa wa taifa wa fainali hizo kwa upande wa klabu ataondoka na Sh.Mil.5, wakati ambapo bingwa kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) atazawadiwa Sh.500,000 na kwa upande wa wanawake bingwa atajizolea Sh.350,000.



























About Author

Advertisement

 
Top