Unknown Unknown Author
Title: Uganda mwenyeji wa CECAFA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kenya imepokonywa fursa ya kuandaa mashindano ya mwaka huu ya kuwania kombe la klabu bingwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati Cecafa, kutoka...
Kombe la CECAFAKenya imepokonywa fursa ya kuandaa mashindano ya mwaka huu ya kuwania kombe la klabu bingwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati Cecafa, kutokana na maandalizi mabaya.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa CECAFA, Nicolasa Musonye, shirikisho la mchezo wa soka nchini Kenya, limeshindwa kuandaa mashindano hayo uamuzi ambao umelazimisha mdhamini mkuu wa mashindano hayo kuipa fursa hiyo shirikisho la mchezo wa soka nchini Uganda, kuyaandaa.
Shirikisho la mchezo wa soka nchini Uganda FUFA, tayari limeteuwa jopo la watu Kumi kuandaa mashindano hayo yatakayo andaliwa katika uwanja wa Namboole mjini Kampala, kati ya tarehe 27 Novemba hadi tarehe 12 Decemba mwaka huu.
Lakini Kenya na Sudan, ambayo inashiriki katika michuano hiyo kwa mara ya kwanza zimepinga uamuzi huo wa CECAFA.

Rais wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Sudan Kusini, Ghabur Goc Alei, amesema atashinikiza nchi wanachama wa CECAFA, kuhakikisha uamuzi uliochukuliwa na kamati kuu ya CECAFA kuhusu mwenyeji wa mashindano hayo unatekelezwa.
Kenya iliteuliwa kuandaa mashindano hayo na kamati kuu ya CECAFA wakati wa mkutano wake ulioandaliwa mjini Dar es Salaam Decemba mwaka uliopita, lakini katibu mkuu wa CECAFA anasema uamuzi huo umechukuliwa baada ya wadhamini wa mashindano hayo kutaka iandaliwe mjini Kampala.




About Author

Advertisement

 
Top