Unknown Unknown Author
Title: TWITE ATUA RASMI JANGWANI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mbuyu Twite (mwenye jezi ya njano) akiongozana na Viongozi wa yanga waliofika kumpokea Uwanjani Twite, Twite, Twite!!!! Hayo ni maneno ...

Mbuyu Twite (mwenye jezi ya njano) akiongozana na Viongozi wa yanga waliofika kumpokea Uwanjani
Twite, Twite, Twite!!!!
Hayo ni maneno ya washabiki wa Yanga walikua wakiimba kumshangilia Twite mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Hakika ilikuwa ni furaha, vifijo na nderemo kwa watu waliofurika kumpokea mchezaji wao mpya Mbuyu Twite.

Mbuyu Twite akiwa na katibu mkuu wa Yanga, Mwesigwa Selestine
Mchezaji mpya wa kimataifa wa timu ya taifa ta Rwanda ,Mbuyu Twite amewasili leo jijini Dar kutokea nchini Rwanda tayari kujiunga na mabingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati timu ya Young Africans.
Twite aliwasali majira ya saa 10:15 kwa majira ya Afrika Mashariki kwa shirika la ndege la Rwanda Air na kupokelewa na viongozi wa Young Africans na washabiki wengi waliojitokeza kumpokea Uwanja wa ndege wa Mwl JK Nyerere.
Mara baada ya kuwasili mlango wa kutokea watu mashuhuri, Twite alipewa jezi ya Yanga yenye namba 4 mgongoni iiiliyoandikwa jina la Aden Rage, mwenyekiti wa Simba.
Umati mkubwa ulijitokeza kiasi kilichopelekea Twite kushindwa kutokea mlango wa kawaida wa kupelekea uongozi wa uwanja huo kumuongoza Twite kutokea mlango wa wageni mashuhuri.
Msafara ulianza Uwanja wa ndege wa Mwl JK Nyerere kuelekea makao makuu ya klabu, huku magari yakiwa mengi, pikipiki na wengine wakitembea kwa miguu mpaka makao makuu ya klabu.
Msafara uliendelea mpaka makao makuu ya klabu, kwa kupitia mtaa wa msimbazi ambapo wapenzi na washabiki wa simba hawakuweza kuamini macho yao mara baada ya kumuona Twite akiwa katika gari ndogo ya Yanga, na washabiki na wanachama wakiwazomea simba na kuwakejeli kwa maneno ya dhihaka.
Umati uliojitokeza kumpokea Mbuyu Twite, Uwanja wa ndge wa mwalimu JK Nyerere








About Author

Advertisement

 
Top