Mbuyu Twite amabye zoezi lake la usajili lilianza takribani wiki mbili zilizopita limefikia mwisho baada ya klabu ya Young Africans kufanikiwa kupata uhamisho wake wa kimataifa kutoka timu aliyokuwa akiichezea ya APR ambapo awali alikuwa akiichezea timu ya st. Lumpopo FC
Twite ambaye alingara sana katika mashindano ya Kagame yaliyomalizika hivi karibuni na Young Africans kuibuka mabingwa, amesema anajisikia furaha na mwenye bahati kufanikiwa kujiunga na mabingwa mara mbili mfululizo wa kombe la Kagame.
Usajili wa Twite ulianza takribani wiki mbili zilizopita ambapo mjumbe wa kamati ya Utendaji wa klabu ya Young Africans Abdallah Bin Kleb aliamua kwenda nchini Rwanda kuhakiksiha zoezi hilo linakamilika haraka ipasavyo, ambapo mara baada ya kumalizana na Twite aliendelea kuhakikisha anafuatilia ITC yake nchini DRC.
Akiongea na www.youngafricans.co.tz Bin Kleb amesema, Young Africans ni timu kubwa katika Ukanda huu, Viongozi wake wanafanya mambo yao kwa uhakika zaidi, hivyo hawakutaka kuongelea suala la Twite mpaka watakapoona wamekamilisha zoezi lote'
"Unajua usajili sio mchezaji kusaini makaratasi ya mkataba tu, kuna kupata barua ya kumruhusu kutoka timu anayotoka, uhamisho wa mchezaji kutoka chama husika cha soka cha nchi, baada ya hapo ndio unaweza kutangaza sasa kwamba ni mchezaji wako halali"alisema Bin Kleb.
Twite anatarajiwa kuwasili mapema wikii kuungana na wacheji wenzake katika mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuaanza septemba mosi.
Tags
Young African FC