Tanzania itafuta sajili ya meli za Iran

Meli ya mafuta ya IranSerikali ya Tanzania inasema meli za mafuta 36 za Iran zimesajiliwa tena nchini Tanzania, ili kujaribu kuhepa vikwazo dhidi ya Iran vilivowekwa na Marekani na Umoja wa Ulaya.

chunguzi uliofaywa na serikali ya Tanzania, ambao ulionekana na shirika la habari la Reuters, unaonesha kuwa serikali haikujua lolote kuhusu shughuli hizo za kuzipatia meli za mafuta za Iran bendera ya Tanzania - shughuli iliyokuwa ikifanywa na wakala alioko Dubai.

Mafuta ya Iran yamewekewa vikwazo, ili kuishawishi Iran iache mradi wake wa nuklia.

Tanzania imeacha kuagiza mafuta kutoka Iran.

Uchunguzi ulifanywa na serikali ya Tanzania, baada ya mbunge mmoja wa Marekani, Howard Berman, mwenyekiti wa kamati ya Congress ya maswala ya nchi za nje, kueleza wasiwasi wake juu ya meli hizo za Iran kupatiwa bendera ya Tanzania.

Tanzania sasa inasema itafuta usajili wa meli hizo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post