NIJUZE NIJUZE Author
Title: Habari za usajili Ligi kuu ya England
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mwezi Agosti Wigan Athletic Klabu ya Wigan Athletic imekamilisha usajili kwa kutiliana saini na mchezaji Ivan Ramis kutoka klabu ya Mallo...
Mwezi Agosti
Wigan Athletic

Klabu ya Wigan Athletic imekamilisha usajili kwa kutiliana saini na mchezaji Ivan Ramis kutoka klabu ya Mallorca kwa kitita cha takriban Euro milioni 6. Beki huyo mwenye umri wa miaka 27 alitarajiwa kujiunga na West Ham baada ya tangazo la Mallorca kudai kua wamekubaliana na West Ham juu ya beki huyo lakini yeye binafsi akafikia makubaliano na Wigan kwa mkataba wa miaka mitatu. Ramis ameichezea Mallorca mara 103 katika La Liga ya Uhispania tangu mwaka 2004. Huyu ni mchezaji wa pili kusajiliwa na kocha Roberto Martinez baada ya Fraser Fyvie kutoka Aberdeen.
Everton
Malipo ya Pienaar yaafikiwa

Klabu ya Everton imeafikiana malipo kwa mcheza kiungo wa klabu ya Tottenham Hotspur Steven Pienaar. Klabu hiyo inayochezea kwenye uwanja wa Goodison Park imekua na hamu kumsajili mchezaji wake hapo zamani ikiwa alihamia Tottenham kutoka Everton mwezi Januari mwaka 2011. Pienaar alirudi Everton kwa mkopo mnamo mwezi Januari mwaka 2012 baada ya kushindwa kufikia viwango vya Spurs. Lakini aliporejea Everton alishiriki mechi 14 akifunga mabao 4 na kuibua kipaji kilichomfanya kuwa nyota katika mwaka 2007.
unior Hoilet ahamia QPR
QPR imemsajili mcheza winga ya kushoto Junior Hoilett kwa mkataba wa miaka minne kutoka klabu ya Blackburn Rovers. Huyu ni mchezaji wa saba kusajiliwa na kocha Mark Hughes, akifuata wachezaji Rob Green, Ryan Nelsen, Fabio Da Silva, Ji-Sung Park, Samba Diakite na Andy Johnson. Kijana huyo kutoka Canada alikua huru bila klabu yoyote baada ya kukataa kutia saini mkataba mpya na Blackburn Rovers, kufuatia klabu hio kushuka daraja hadi mashindano ya Championship.
Vlaar ajiunga na Aston VillaAston Villa imekamilisha usajili wa beki wa klabu ya Feyenoord Ron Vlaar kwa mkataba wa miaka mitatu akisubiri kukamilisha utaratibu wa afya wiki hii.
Vlaar alikua kwenye kikosi cha Uholanzi wakati wa mashindano ya Euro 2012, na alikua huko Villa Park hivi karibuni kwa majadiliano na kocha mpya Paul Lambert. Beki huyo anatazamiwa kupitia utaratibu wa afya jumatatu kukamilisha usajili wake kutoka klabu ya Feyernoord.
Chelsea yakamilisha usajili wa Oscar.
Klabu ya Chelsea imehitimisha usajili wa mcheza kiungo kutoka Brazil Oscar aliyekua akichezea klabu ya Internacional kwa kitita cha Euro milioni €32m. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 yuko kwenye kikosi cha Taifa cha Brazil kinachoshiriki mashindano ya Olimpiki.
Oscar alianza kucheza soka akiwa katika klabu ya Sao Paulo kabla ya kuhamia Internacional mnamo mwaka 2010. Katika kipindi hicho alifunga mabao 11 katika mechi 36 za Ligi.
Chelsea vilevile imemsajili ndugu yake nyota Hazard kutoka Ufaransa aliyesajiliwa na klabu hio mapema Thorgan Hazard.
Tottenham.
Mpango wa Modric kujiunga na Real Madrid bado una ati atiTottenham-v-Everton-Aaron-Lennon-Luka-Modric_2701094
Meneja wa Tottenham Andre Villas-Boas ameonya vilabu vinavyomtaka kiungo wake Luka Modric kua kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 haondoki hadi anayemtaka atimize kitita cha pauni milioni 35 ilichodai Spurs. Kwa kipindi cha mwaka mzima majaliwa ya kiungo huyo yamekua gumzo ambapo Real Madrid imeongoza kwa vilabu vinavyomtaka ajiunge navyo. Lakini Real Madrid imeshikilia msimamo wa kua hawazidishi pauni milioni 27.











About Author

Advertisement

 
Top