NIJUZE NIJUZE Author
Title: ZAIDI YA WATOTO 1000 NCHINI WANUFAIKA KUPATA ELIMU KWA MSAADA WA “WAMA”
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Zaidi ya watoto wa kike na wa kiume elfu moja ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kutoka mikoa yote nchini wamenufaika...
image Zaidi ya watoto wa kike na wa kiume elfu moja ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kutoka mikoa yote nchini wamenufaika na ufadhili wa masomo unaotolewa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) iliyopo jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo na mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo wakati akiongea kwenye mkutano wa saba wa wake wa marais wa Afrika uliozungumzia masuala ya amani barani Afrika uliomalizika leo mjini Abuja nchini Nigeria.
Mama Kikwete alisema kuwa kati ya wanafunzi waliopata ufadhili huo 532 wanasoma elimu ya Sekondari katika shule mbalimbali hapa nchini, 250 wanasoma shule ya  Sekondari ya mfano ya wasichana inayomilikiwa na Taasisi hiyo ya WAMA-NAKAYAMA iliyopo Rufiji Mkoani Pwani na wanafunzi 12 wanasoma vyuo vya elimu ya juu.
“Taasisi yangu imejenga Shule ya Sekondari ya kata inayomilikiwa na Serikali ya Nyamisati pamoja na nyumba za walimu ambapo jumla ya wanafunzi 320 wanasoma katika shule hiyo, pia tumeweza kujenga mabweni ya wasichana katika shule mbalimbali za sekondari.

Tumechangia elimu kwa kutoa vitabu milioni moja, madawati, vitanda, magodoro na kufunga umeme wa jua kwenye baadhi ya shule zisizokuwa na umeme”, alisema Mwenyekiti huyo wa WAMA”, alisema Mwenyekiti huyo wa WAMA. Kwa upande wa afya, Mama Kikwete alisema kuwa kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) wamekuwa wakitumia kampeni ya mtoto wa mwenzio ni wako mkinge na maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, ambayo lengo lake kuu ni kupunguza maambuikizi ya ugonjwa huo kwa watoto na vijana.

Pia Taasisi hiyo imetoa vifaa mbalimbali vya afya ili kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali 71, kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na umuhimu wa mpango wa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) katika mikoa ya Tabora, Pwani, Kagera, Kigoma na Mtwara.

Mama Kikwete alisema, “Tumeweza kuwasaidia na kuwainua wanawake kiuchumi kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali na kutoa msaada wa kifedha kwa vikundi 89 vya Benki za maendeleo vijijini (VICOBA) na Vikundi vya kuweka Akiba na Kukopa (SACCOs), kutoa mafunzo ya ukulima wa zao la pilipili aina ya Paprika kwa wakulima 134 na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake 400 katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.

Alimalizia kwa kusema kuwa, Taasisi ya WAMA imeweza kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa maafisa maendeleo ya jamii katika mikoa ya Lindi ambao waliweza  uvifundisha vikundi vya wanawake katika maeneo ya vijijini, kutoa mafunzo ya Ukimwi na virutubisho vya mwili kwa wanawake 100 na usindikaji wa vyakula kwa wanawake 120 katika mikoa ya Arusha na Pwani.

Taasisi ya WAMA ilianzishwa mwaka 2006 huku ikiwa na malengo ya kumuinua mwanamke kiuchumi, kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanaotoka katika mazingira hatarishi wanapata elimu na kuimarisha afya ya mama wajawazito na watoto.

About Author

Advertisement

 
Top