MKUU WA WILAYA YA NACHINGWEA MKOANI LINDI,BI REGINA CHONJO AKIONGEA NA MAKUNDI MBALIMBALI KATIKA UKUMBI WA TTC NACHINGWEA BAADA YA MKUTANO ALIPATA FURSA YA KUPIGA PICHA YA PAMOJA NA AKINA MAMA Bint Kanduru(tshirt ya CCM ya njano) akisikiliza kwa umakini maelezo ya mkuu wa wilaya...Bibi huyo ni Mzee Mashuhuri aliyejitolea kupigania Uhuru wa Nchi hii na Bado nitegemeo kubwa kwa shughuli za kuhimiza maendeleo wilayani humo Wazee na vijana waliojitokeza kumsikiliza Mkuu wa wilaya hiyo Na wao kupata fursa ya kubadilishana mawazo ili kuleta maendeleo wilayani humo
MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Bi Regina Chonjo amesema kuwa kauli mbiu yake katika kuhimiza maendeleo wilayani humo ni amani na maendeleo ambayo inahimizwa kwa wakazi wote wa wilaya hiyo wenye uwezo wa kufanya kazi na amewatahadharisha wananchi kuona umuhimu wa kufanya kazi mbalimbali zitakazoweza kuwaletea kipato
Akiongea na Makundi mbali mbali yakiwemo ya Wazee,akina mama na walemavu wilayani humo,Chonjo Alisema kuwa maendeleo kila mkazi mwenye uwezo wa kufanya kazi ni lazima awajibike kikamilifu ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wakazi wote wa wilaya hiyo kwa kuelekeza nguvu kwa kuhakikisha wananchi wanaondokana na ujinga, maradhi na umasikini.
Aliendelea kufafanua kuwa ujinga ndio unaathari kubwa hivyo mtazamo wake utakuwa ni kusimamia swala zima la Elimu hasa ikizingatiwa kuwa kila kata kuna shule za msingi na sekondari hivyo watoto wenye umri wa kwenda kuanza shule ni lazima wazazi wao wawapeleke kwenye shule ili kuondokana na tatizo sugu la ujinga na wanafunzi ambao wanaonekana kuwa hivyo kwa kuchangiwa na Wazazi kutohamasika na Elimu wilayani humo
Alieleza zaidi kuwa amewaagiza maafisa watendaji wa kata zote kuhakikisha kuwa wanawasiliana na wakuu wa shule za sekondari za kata ili kuwabaini wanafunzi watoro ambao wanapaswa warejee kwenye shule zao kabla ya hatua zingine kuanza kuchukuliwa.
Amewaonya baadhi ya Wananchi wasiopenda kujitolea kuchangia Maendeleo ya Wilaya hiyo ambayo tayari awali ilifanikiwa kwa kujenga ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri kwa kuchangia na kujitolea nguvu zao hadi kukamilika
Wilaya ya Nachingwea wananchi wake ni wakulima,hivyo kazi kubwa mbele yake ni kuhakikisha kuwa wilaya hiyo inakuwa na mazao ya chakula na biashara ambapo aliyataja mazao ya chakula kuwa ni mahindi, muhogo na mpunga na mazao ya biashara ni korosho na Ufuta huku Mbaazi na Choroko zikisaidia kuingiza pato kubwa.
Alibainisha zaidi kuwa vijana wote katika wilaya hiyo wenye uwezo ni lazima wafanye kazi bila kuchagua kazi na waachane na swala la kunywa pombe nyakati za saa za mchana na badala yake waone umuhimu wa kubuni miradi mbalimbali za maendeleo zitakazo weza kuwakwamua kiuchumi.
Aidha amewahimiza wawekezaji hapa nchini kuona umuhimu wa kuwekeza katika maeneo mbalimbali kufuatia wilaya hiyo kuwa na Madini ya aina mbalimbali pamoja na Ardhi ya kutosha kuwekeza katika kilimo
Tayari ofisi yake inaandaa maombi kwa Serikali kupanga mipango ya Kurudisha usafiri wa Reli ambao ulikuwapo miaka ya nyuma katika wilaya hiyo ili kusaidia Usafirishaji wa Mazao kama ilivyokuwa awali ambapo tuta la Reli hiyo bado lipo ambapo itasaidia kupunguza gharama na urudishwaji
Picha na Habari: ABDULAZIZ ....LINDI