WAIGIZAJI Mahiri katika tasnia ya filamu nchini Jacob Stephen ‘JB’ na Aunty Ezekiel wamechaguliwa kuwa mabalozi wa channel ya Zuku Swahili Movie Channel itakayokuwa ikirusha filamu zinazotumia lugha ya Kiswahili, sehemu kubwa ya filamu hizo zitakuwa ni zile zilizosambazwa na kampuni ya Steps Entartainment ya jijini Dar es Salaam alisema mkurugenzi wa Zuku kwa upande wa Tanzania, Johnson.
“JB na Aunty Ezekiel wamepata nafasi ya kuwa mabalozi wa Zuku Swahili movie kwa Tanzania, hii ni hatua moja mbele kwa maendeleo ya filamu Swahiliwood, lakini ni furaha kwa wasanii wenyewe kwa Zuku kuwachagua kuwa mabalozi wa channel inayoonyesha kazi zao za filamu, lakini pia Zuku inakusudia kukuza lugha ya Kiswahili kwa kupitia channel hiyo,” anasema Johnson.
Uzinduzi rasmi wa Zuku Swahili Movie Channel utafanyika mwezi wa nane, channel hiyo utaiona kwa kupitia king’amuzi cha ZUKU.