Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijja amesema kuwa Serikali itaendelea kukiwezesha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ili kiendelea kuzalisha wataalam mbalimbali watakaochangia kuleta maendeleo nchini. Khijja ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es salaam mara baada ya kuzindua maadhimisho ya miaka 40 tangu Chuo hicho kilipoanzishwa mwaka 1972 kwa lengo la kuzalisha watalaam wa kada mbalimbali. Alisema kuwa Chuo hicho kimeendelea kuwa muhimu katika kuwaendeleza vijana na hata watumishi waliopo kazini na hivyo kuboresha kada mbalimbali ikiwemo elimu juu ya masuala ya bima na fedha. Hivyo ametoa wito kwa wazazi kuendelea kuwapeleka watoto wao katika Chuo hicho kwa ajili ya kupata utalaam ambazo utawasaidia wao binafsi na Taifa kwa ujumla. Khijja alisema katika ya sasa ni vema wazazi wakawapatia watoto wao elimu kwani ndio itakayowakomboa.
Home
»
»Unlabelled
» IFM YATIMIZA MIAKA 40 TANGU KUANZISHWA MWAKA 1972
About Author
JE, UNA HABARI, PICHA, TANGAZO, MAKALA NA USHAURI? USISITE KUWASILIANA NASI SIMU / WHATSAPP NAMBA 0625535420.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.