Mchezaji Dan Wagaluka wa timu ya APR ya Rwanda, akiumiliki mpira mbele ya Hamis Kiiza wa Yanga, wakatawa mchezo wa nusu fainali wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mabingwa watetezi wa michuano ya kagame yanga wametinga hatua ya fainali baada ya kuifunga apr ya rwanda kwa bao 1-0. Mchezo huo uliyocheza kwa dakika 120 baada ya muda wa kawaida kumalizika huku kila timu zikitoka 0-0. Katika mchezo huo uliyovuta hisia za watu wengi kutokana mechi ilivyokuwa.Mwamuzi anthony ogwayo alimtoa kwa kadi nyekundu mchezaji godfrey taita baada ya kuchelewesha mpira kwa makusudi. Dakika ya 99 ya mchezo mchezaji hamis kiiza ameipatia yanga bao akimalizia krosi ya haruna niyonzima. Mchezo huo uliongezwa dakika 30 baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika huku zikitoka bila ya kufungana.
Mpaka mapumziko si yanga wala apr iliyopata bao. Katika kipindi hicho mchezaji leonel st. Preus alikosa bao la wazi katika dakika ya 10 ya mchezo baada ya kupiga shuti kali lililogonga mwamba na kutoka nje.
Dakika ya 15 ya mchezo nusura chuji aipatie yanga bao la kuongoza baada ya kupiga shuti lililookolewa na kipa wa apr. Kwa ujumla kipindi hicho kilikuwa cha mashambulizi makali huku kipa wa yanga ali mustafa akionekana shujaa kwa kuweza kupangua mipira mingi ya hatari.
Wachezaji taita, kiiza na shamte walipata kadi za njano baada ya kucheza vibaya. Yanga ilifanya mabadiliko ametoka juma abdul na nafasi yake kuchukuliwa ba shamte ali.
VIKOSI VYA LEO
YANGA- Ali mustafa, nadir haroub, kevin yondani, haruna niyonzima, juma abdul/shamte ali, athuman iddy chuji' oscar joshua, hamis kiiza,david luhende, said bahanuzi na godfrey taita.
APR-Ndoli clayde, karekezi olivier, seleman ndikumana,mugiraneza jean,jonson bagoole, leonel st.preus,iranzi claude,mbuyu twite, dan wagaluka
na tuyizere donatien