MISS EAST AFRICA 2012 (MALAWI)

Miss Elidas Ella Chirwa (22)

Mrembo atakayeiwakilisha Nchi ya Malawi katika mashindano ya Miss East Africa 2012 ametangazwa rasmi baada ya kuwashinda wenzake 39 waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Malawi katika mashindano hayo.

Mrembo huyo ni Miss Elidas Ella Chirwa (22) mwenye urefu wa 1.82m ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo kikuu cha Malawi

Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.

Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post