KINA MAMA WAENDELEZA UTUPAJI WA WATOTO WACHANGA-MBEYA

Mtoto huyu amekutwa ametupwa akiwa amefariki huko maeneo ya msikiti wa Soweto jijini Mbeya leo Asubuhi!! Tunaomba Radhi kwa picha mtakazoziona.

Picha hizo mbili zinamuonyesha mtoto huyo ambaye hakuweza kufahamika jina lake wala mama yake, akiwa ametolewa kwenye mfuko wa Salfet aliokuwa amehifadhiwa na kutupwa, hiyo khanga ni kutoka kwa msamaria mwema
Polisi akiwa wanaonekana anaondoka na Mwili wa Marehemu eneo la tukio
Katika hali ya kutatanisha wananchi wa Soweto jijini Mbeya wamekutana na Kifurushi ambacho ndani yake kulikuwa na mtoto mchanga amewekwa na kutupwa akiwa amefariki, ikiwa ni tukio la pili kutokea eneo hilo baada ya tukio kama hilo kutokea wiki mbili zilizopita.
Hata hivyo akiongea na baadhi ya wananchi ambao hawakupenda kutaja majina yao wamedai kwamba kuna dispensary jirani hapo ambayo hawakutaka sema ni hospital ipi ambapo wana wasi wasi kwamba hutoa Mimba mabinti na kuwatupa eneo hilo.
uchunguzi wa kina unafanyawa ilikujua kama ni kweli maelezo ya wadau na tunafuatilia kama kweli Dispensary hiyo ipo.Polisi wakiondoka eneo la tukio

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post