Umaskini uliokithiri miongoni mwa wazazi na walezi pamoja na mila na desturi zilizopitwa na wakati kumeelezwa kuwa ni chanzo cha kuongezeka kwa tatizo mimba za utoto mkoani Lindi
Hayo yamebainishwa w kwenye mkutano wadau wa afya ya uzazi na stadi za maisha ulioendeshwa na shirika lisilo la kiserikali Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwa kushirikiana na Engenderhealth kwa ufadhili wa USAID uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa jana.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wengine afisa utamaduni katika Manispaa ya Lindi Maneno Juma alisema kutokana kukithiri kwa umaskini wazazi wengi wanashindwa kuwathibiti mabinti zao kwa vile huwatumia hao kuwa chanzo cha mapato kwa ajili ya kuendesha familia.
Alisema kuwa kutokana na wazazi kushindwa kukemea vitendo vichafu ikiwemo kushiriki mapenzi vinavyo fanywa na mabinti zao wakiwemo mapenzi kwa wanafunzi wa shule za sekondari na hivyo kusababisha kupata mimba wakiwa kwenye umri mdogo.
Alisema wazazi na walezi wamekuwa na tabia ya kutokemea vitendo vya Watoto kutoka nyumbani nyakati za usiku na kurudi asubuhi wakiwa na zawadi mbalimbali na fedha ambazo uwaziba midomo washindwe kukemea tabia hiyo chafu.
Nae Fatuma Shomali alisema wazazi au walezi wengi siku hizi wameacha kufuata maadili ya dini na mila ya kukaa pamoja na Watoto wao wa kike kwenye moto ya jioni na kuwafunda kwa kuwakanya kutenda matendo yasiyo kuwa yenye maadili mema.
Shomali alisema pia wazazi hao wanashindwa kutumia nafasi ya uzazi kwa kuwakemea Watoto wengine ambao sio Watoto wao pale wanapowakuta wanatenda matendo yasiyo fuata maadili mema.
MWANJA IBADI Lindi
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.