Hayo yamebainishwa na afisa mradi wa elimu rafiki kwa vijana Diana Karioki wa shirika la Mariestopes tawi la Mtwara wakati alipokuwa anafanya majumuhisho baada ya kukamilika kwa utoaji wa huduma za uelimishaji vijana , upimaji wa virusi vya ukimwi na huduma za mpango wa uzazi uliofanyika katika kata tano za manispaa hiyo.
Diana alisema kuwa katika kipindi cha siku tano baada ya uzinduzi waliweza kuwafikia wanawake 366 ambao walipata huduma za uzazi wa mpango na upimaji virusi vya ukimwi .
Alisema Wanawake 297 walipata huduma ya uzazi wa mpango na 147 walichagua huduma ya vipandikizi ambavyo hudumu kwa miaka mitatu, 91 huduma ya sindano na 59 walipata vidonge.
Afisa mradi huyo alisema kati ya watu 250 waliojitokeza kupima ukimwi pekee 190 walikuwa wanawake ambapo watano kati yao walibainika kuambukizwa na virusi vya ukimwi, na wanaume 60 walikuwa ni salama.
Alisema vijana ambao ndiyo walengwa katika mradi huo hawakujitokeza kwa wingi kama ilivyotazamiwa kutokana kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya elimu rafiki kwa vijana inayoendeshwa na mariestopes.
Kwa mujibu wa taarifa mratibu wa ukimwi mkoa wa Lindi Magege s magege kutokana na utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria kwa kipindi cha mwaka 2007/08 kuwa kiwango cha maambukizi ya ukimwi mkoani humo yako kwa asilimia 3.8 wakati manispaaa ya Lindi inaongozwa kimkoa kwa asilimia 8.9.
Magege alisema kuwa wilaya inayofuata kwa maambukizi ni Ruangwa 3.8 Nachingwea kwa asilimia 3.6 Liwale 2.3 Kilwa 2.3 na Lindi ni asilimia 2.0.
Mwanja Ibadi Lindi
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.