Iran yaunda ndege isiyohitaji rubani

111214062124_us_drone_304x171_reuters_nocredit Iran inasema imeanza kuunda ndege ya ujasusi sawa na ile ya aina ya Sentinel ya Marekani, ambayo ilianguka nchini Iran mwaka jana.

Wakuu wa Iran wanasema wamepata maelezo kuhusu namna ndege hiyo inavofanya kazi, kwa kufumbua fumbo la software yake; na sasa inaelewa kikamilifu muundo wa ndege hiyo.

Kuna wasiwasi kuwa Iran huenda ikaweza kuigiza rangi maalumu ambayo inasaidia kufanya ndege hiyo isionekane na vyombo vya radar.

Ndege hiyo ya aina ya Sentinel isiyohitaji rubani, inatumiwa sana na Marekani kugundua maficho ya makundi ya wapiganaji nchini Afghanistan na Pakistan.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post