KINARA wa filamu za mapenzi na matukio ya kusisimua bongo, Aunty Ezekiel, amesema anajipaga kuja na ujio mpya mwaka 2012, huku akiwashukuru mashabiki wake kwa kumsapoti kipindi chote cha miezi 12 inayoenda kumalizi hivi karibuni.
Akizungumza na DarTalk, msanii huyo alisema mara nyingi amekuwa akifanya filamu kwa malengo na mikakati hivyo tayari kichwa chake kinawaza hapo mwakani anatafanya kazigani ya kwanza ambayo itaamsha hisia kwa mashabiki wake.
Alisema mikakati yake ya hapo mwakani ni kucheza filamu nyingi hasa za kimataifa ambazo anaamini zitaweza kuinua kipaji chake na kufika mbali zaidi ya hapo alipo sasa.
"Kila mtu huwa anafanya kitu kwa malengo kwangu mimi tayari nimeshajiwekea kazi ambazo nitazifanya mwakani hivyo naweza kusema kuwa nataka kucheza filamu nyingi za kimataifa ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kufungua njia ya mafanikio zaidi kuliko haya nilinayo sasa," alisema.
Aliongeza kuwa mbali na yeye kuwa na mikakati hiyo pia anawashauri wasanii wengine kuwa wafanye kazi kwa malengo na siyo bora kuonekana wanafanya kazi lakini hazina manufuaa yoyote katika maisha yao ya baadae.
Tags
BOLYWOOD