Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy Mapunda akikabidhi kombe kwa viongozi wa timu ya Bunge na Timu ya Baraza la Wawakilishi.Pichani kulia ni Kapteni wa timu ya Bunge,Mh Amos Makala na kushoto ni Mwenyeki wa timu ya Baraza la Wawakilishi,Mh Hamza Hassani Juma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy,Mapunda akizungumza mbele ya wanahabari mapema leo Makao Makuu ya ofisi hizo zilizopo Oysterbay,jijini Dar,kuhusiana na udhamini wa mechi kati ya Timu ya Wabunge na Timu ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar,itakayofanyika 9 Desemba kwenye Uwanja wa Uhuru,ikiwa ni sehemu mojawapo ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru,aidha Teddy amesema kuwa udhamini wa timu hizo umegharimu kiasi cha zaidi ya milioni 65.
Tags
TANZANIA