Muda
wa Nicolas Anelka na Alex kuwa Stamford Bridge umeisha baada ya kocha Andre
Villas-Boas kutangaza kuwa amekubali maombi ya wachezaji hao kutaka
kuondoka Chelsea.
Wachezaji
hawa wawili hawakuwa wamewekwa katika kikosi kilichosafiri kuelekea
ST.James Park leo hii, na jana waliripotiwa kupigwa stop na AVB
kushiriki katika mazoezi ya kikosi cha kwanza.
Chelsea wamethibitisha juu ya hatma ya Anelka na Alex mara tu baada ya timu hiyo kushinda mechi yake ya dhidi ya Newcastle.
Villas-Boas
alisema: “Mazungumzo yangu na wachezaji(Anelka na Alex) yalikuwa fair
and direct. Walionyesha nia ya kutaka kuondoka hapa, na wakaomba kupitia
transfer request kwa muda sasa.
“NI
wachezaji wa daraja la juu, ma-pro wa ukweli wasiona mashaka, lakini
kwa muda huu na matokeo ya hivi karibuni, tumeamua ya kuyakubali maombi
yao ya kutaka kuondoka ili kujaribu kupata wachezaji wengine watakaojaza
nafasi zao kuweza kuimarisha kikosi chetu.”
Tags
Usajili Barani Ulaya